Showing posts with label MAKALA. Show all posts
Showing posts with label MAKALA. Show all posts

Friday, 27 January 2017

Mke fanya haya kwa mume wako

Itunze Ndoa Yako MKE, FANYA HAYA KWA MUME WAKO. 1. Muite kwa jina lake la utani 2. Muache atumie mamlaka yake kama kichwa cha nyumba. 3. Usimcheke akiwa ameumizwa na jambo fulani. 4. Kaa kimya pale anapokuwa na hasira. Unaweza ukaenda kumuomba msamaha na kumueleza kwanini ulimkosea pale hasira zinapokua zimemuisha. 5. Kuwa na haraka ya kuomba msamaha pale unapokosea, sisitiza juu ya msamaha na mbusu pale anapokusamehe. 6. Ongelea mazuri yake na yeye kabla ndugu, jamaa na marafiki hawajafanya hivyo. 7. Waheshimu wazazi wake. 8. Msisitize kuhusu kwenda kuwasalimia wazazi wake na kuwapelekea chochote. Na afanye hvyo na kwa wazazi wako pia. 9. Msuprise kwa chakula akipendacho, hasa kipindi kile anapokuwa na msongo wa mawazo. Na kamwe usimcheleweshee chakula chake. 10. Usiruhusu dada wa kazi amhudumie chakula mume wako ukiwa nyumbani. 11. Mkaribishe kwa kumkumbatia anapotoka kwenye mihangaiko yake. Msaidie mizigo aliyokuja nayo au hata begi. 12. Tabasamu pale unapomtizama, vaa vizuri na jipendezeshe pale mnapotoka wote kwenda kwenye warsha mbalimbali. 13. Mpigie simu na umwambie kwamba unampenda na umemkumbuka 14. Muamshe asubuhi na umpe romance kiasi kwamba ifike hatua ya kuhitaji, mpe na hata jishughulisha na wanawake wengine siku hiyo. 15. Kamwe usithubutu kutamka kuwa hakuridhishi na tendo la ndoa. Tafuta njia muafaka ya kufikisha ujumbe wako. 16. Mwambie ni kiasi gani una bahati kuwa nae kama mume wako. 17. Mkumbatie tu bila sababu yoyote ile. 18. Mshukuru Mungu kwa kukupa Adamu wako katika maisha yako. 19. Kumbuka kumuombea na kumkabidhi mikononi mwa Mungu. 20. Tengenezeni utaratibu wa familia nzima kumshukuru Mungu kwa pamoja kila asubuhi na usiku kabla ya kulala. Mungu abariki ndoa yako. Mlio single Mkapate wapenzi wenye mapenzi ya kweli leo na daima. Na wasio serious na mahusiano wanaokupotezea muda wako wajikatae kwako mapema ili wasikuzibie nafasi ya kutimiza kusudi la Mungu kwako. Kwanini tusiseme "Amen"! Share

MADHARA ya mionzi ya simu

Simu yako ni HATARI SANA kwenye Afya yako. Fuhamu MADHARA yatokanayo na simu yako na JINSI YA KUYAPUNGUZA. Simu tunazozitumia hutoa mionzi (radiations) hatari sana ijulikanayo kama "Electromagnetic waves" wakati wa kupiga/kupokea simu, kuperuzi Internet, nk.. Madhara ya Mionzi hii; 1. Husababisha Saratani ya Ubongo (Brain Cancer) na ngozi (Skin Cancer). 2. Husababisha hitilafu kwenye Ubongo na hii hupelekea kupoteza kumbukumbu, uwezo mdogo wa kupambanua mambo na umakini (Concentration). 3. Husababisha upungufu wa mbegu za kiume na hata utasa (Impotence) kwa wanaume. 4. Huongeza shinikizo la damu. Jinsi ya kupunguza Athari zitokanazo na Mionzi hii hatari; 1. Weka vifaa maalum vya kupunguza mionzi (Radiation absorbers) kwenye simu yako. Vinapatikana madukani. 2. Usipende kuweka simu mfukoni endapo huitumii. Wakati wa kulala weka mbali angalao SM 30 kutoka ulipo. 3. Simu iwapo mfukoni, upande wa Vitufe na kioo cha simu ndio kielekee mwili wako! 4. Tumia "headsets" au "Kipaza sauti (Loud Speaker). Hii hukusaidia kuwa mbali na mionzi wakati wa kupiga/kupokea simu. 5. Usiitumie simu yako iwapo ina "bar" moja au mbili za "network" (Low Network Signal). Wakati huu simu inafanya kazi kupita kiwango cha kawaida hivyo huongeza wingi wa mionzi. 6. Wakati wa kupiga simu, subiri ipokelewe ndio uisogeze karibu ya mwili (mf. Masikioni). 7. Iwezekanapo, penda kuwasiliana kwa ujumbe wa maneno (text msg) kulipo kupiga simu. Simu ni muhimu sana katika Maisha yetu ya sasa. Hutuunganisha na ulimwengu uliogubikwa na Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia. Sanjari na hili, tunapaswa kuwa makini katika juhudi za kujaribu kuepuka Madhara yatokanayo na simu kama ilivyoainishwa hapo juu. #plusJrPositeveMimd NOTE: Share kwa wengine wajifunze.

Kisa cha kusisimua

KISA CHA KUSISIMUA Kuna kijana mmoja daktari alikwenda kuposa. Binti aliyemposa akamuwekea masharti mazito. Akamwambia chagua mawili imma kunioa mimi au kukaa na mama yako, kwa sababu ukinioa mimi sitokubali mama yako aje hata harusini kwangu! Yule kijana aliemewa. Hakujua la kufanya. Mke anamtaka, lakini mama yake pia anampenda. Hivyo aliamua kuomba ushauri kwa mwalimu wake wa chuo kikuu. Alimwambia: moyo wangu unampenda mno binti niliyekwenda kumposa, lakini pia siwezi kuishi mbali na mama yangu. Nifanye nini? Yule mwalimu mwenye hekima ambaye alikuwa anajua tabu alizopitia mama wa kijana yule, alimjibu kwa kumwambia: Kabla ya kukueleza uchague yupi kati ya wawili hao, rudi nyumbani, na leo usifanye chochote, ila kuikosha mikono ya mama yako. Yule kijana alifanya kama alivyotakiwa na mwalimu wake. Alipofika nyumbani aliomba idhini kwa mama yake amruhusu kuikosha mikono yake, na yule mama alimkubalia bila ya ajizi yoyote. Yule kijana alipoanza kuikosha mikono ya mama yake na kuona jinsi ilivyogugutaa kwa kazi za sulubu, alilia sana. Muda wote huu alikuwa hajawahi kuangalia viganja vya mama yake. *Je, na wewe umewahi kukaa na kuangalia viganja vya mama au baba yako kuona tabu walizopitia kukulea?* Kumbe baba wa yule kijana alifariki dunia yeye akiwa bado mdogo, yule mama aliamua kusamehe kila kitu kwa ajili ya mustakbali wa mwanawe. Alijitolea kufanya kazi za sulubu. Alikubali kuwa mtumishi wa ndani, kukosha nguo, kupiga deki na kila kazi ambayo alihisi ingelimletea chumo la halali bila ya kujali ugumu wa jkazu hiyo. Juhudi zake zilizaa matunda na kufanikiwa kumlea na kumsomesha mwanawe hadi chuo kikuu na sasa ni daktari ambaye ana mustakbali mzuri. Baada ya yule kijana kukumbuka yote hayo, alifanya haraka kumpigia simu mwalimu wake huku macho yakiendelea kububujikwa na machozi akimwambia, siwezi kusubiri hadi kesho. Jibu nimeshalipata. Siwezi kumtupa mama yangu kwa ajili ya mtu asiyejua thamani ya mama. Ahsante sana kwa kunionesha njia sahihi! Kamwe siwezi kumuuza mama yangu kwa ajili ya leo yangu wakati yeye ameuza maisha yake yote kwa ajili ya mustakbali wangu. NANI KAMA MAMA?!? Maa! Tabasamu lako ni ufunguo wangu wa ofanisi. Kama umeipenda. Share kwa wengine ili nao wazinduke.

Kisa cha kusisimua

Binti wa miaka 19 ambaye aliacha shule baada ya baba na mama kufa katika ajali mbaya na ndugu kutompa msaada aliamua kuondoka nyumbani na kwenda kuishi na kijana mmoja. Miaka 10 sasa amekuwa anakaa na rafiki yake wa kiume avutaye bangi katika ghetto. Amekuwa anapewa fedha kidogo kutoka kwa huyo mpenzi wake ili anunulie chakula na kula na marafiki wa kaka huyo baada ya kutumika kimapenzi kwa wiki zima huku akiuza maji ya kunywa. Baada ya muda akajikuta ni mjamzito na huyo kijana akamwambia watoe tu mimba hiyo.Akampa fedha kidogo na kumwambia aongeze nyingine ambazo amekuwa akimpa ili akatoe mimba bila kukumbuka kuwa fedha hizo zimekuwa zikitumika kwa ajili ya chakula. Siku ya pili yake akiwa anatoka chumbani mwao kwenda kutoa mimba, akpita kwenye korido ambako akakanyanga sakafu ambayo ina maji na kuteleza. yule kijana akamwona wakati anaangukia tumbo pale sakafuni na akasema, “ amini au usiamini hii ndio njia rahisi niliyoitaka uitumie kutoa mimba hiyo” Kijana akamchukua binti wakati huo damu nyingi zikimtoka na kumwambia aende bafuni akanawe.Lakini kwa nguvu za mwenyezi Mungu yule dada alipona ingawa mimba ilitoka na akaumwa kwa zaidi ya wiki bila msaada wowote ule.. Siku moja akiwa anauza maji akakutana na muuza magazeti na kumpa maji pakiti moja bure na kumwambia, “leo ni miaka kumi tangu baba na mama yangu wafariki katika ajali mbaya, hivyo sitajali mchumba wangu atasemaje au kunifanya nini kwa kutoa maji haya bure, ila mimi nitatoa maji bure kama kumbukumbu ya siku hii yenye simanzi kwangu”. Akiwa anataka kuondoka yule muuza magazeti akamwambia kuwa kuna nafasi ya kazi sehemu na kuwa atamsaidia kuandika barua ya kuomba. Yule dada ailishukuru na akawa anampigia mara kwa mara yule muuza magazeti mpaka siku akaitwa kwenda kwenye usaili. Siku ya usaili akiwa njiani anaelekea huko akakutana na mama mmoja akiwa na gari aina ya BMW likiwa nimeishiwa mafuta. Yule dada akamuuliza mama, Je unahitaji msaada gani? yule mama akamwambia nimeishiwa mafuta na sijui cha kufanya hapa. Dada akachukua kidumu na kwenda mbio kumnunulia mafuta yule mama na akarudi na kumpa. Yule mama alipotaka kumpa hela, dada akakataa akasema nimekuona nikamkumbuka mama yangu hivyo nimefurahi kukusaidia, kama hutajali naomba niwahi sehemu. Kufika kwenye usaili dada akashangaa kuona kumbe yule mama mwenye BMW ndio boss wa ile kampuni na akafanyiwa usahili na kuanza kazi na sasa anajimudu kifedha na ana biashara zake. Na sasa hakai tena na yule kijana mvuta bangi wakati nusu ya utajiri wake anaupeleka kwenye vituo vya kulelea watoto yatima. Nami leo nakuombea unayeisoma habari hii, Mungu akujalie na kukufungulia milango ya mafanikio katika kila jaribu unalolipitia na ukumbuke kuwasaidia wanao hitaji msaada wako. Comment neno “Amen” na kisha share Huwezi jua madhara ya kuupuuzia ujumbe huu

Wednesday, 14 December 2016

Maisha ya ndoa pata fundisho hili

MAISHA YA NDOA/NDOA NDOANO-PATA FUNDISHO HILI Siku moja katika darasa la jioni la watu wazima, mwalimu wa saikolojia aliingia darasani na kuwaambia wanafunzi; "Nataka tucheze mchezo, mtu yeyote yule naomba ajitolee aje hapa mbele" Mwanamke aitwae Cathy akatoka mbele. Mwalimu akamwambia aandike majina 30 ubaoni ya watu ambao anadhani ni wa muhimu katika maisha yake. Cathy akaandika majina ya wanafamilia yake yaani mumewe na mwanae, ndugu, majirani na marafiki zake. Mwalimu akamwambia Cathy afute majina matatu ambayo anadhani kwake sio ya muhimu sana kuzidi mengine. Cathy akafuta majina ya marafiki zake watatu. Mwalimu akamwambia Cathy afute tena majina matano zaidi, Cathy akafuta majina ya majirani zake watano. Hii iliendelea mpaka alipobakiwa na idadi ya watu wanne tu katika ubao. Haya yalikuwa majina ya wazazi wake, mumewe na mtoto wake wa pekee. Darasa zima wakabaki kimya, baada ya kugundua kuwa huu sio mchezo wa Cathy peke yake sasa. Mwalimu akamwambia Cathy afute majina mengine mawili kati ya yale manne yaliyobaki. Ulikuwa uamuzi mgumu mno kwa Cathy. Bila hiyari akafuta majina ya wazazi wake. "Futa jingine zaidi tafadhali" mwalimu alimwambia. Cathy akaishiwa pozi, na huku mikono ikimtetemeka na machozi katika macho yake akafuta jina la mwanae wa pekee. Na kubakiza jina la mume wake, Cathy alilia mno!!! Mwalimu akamwambia Cathy aende akakae. Baada ya muda kidogo mwalimu akamuuliza Cathy "kwanini mume wako? Wazazi wako ndio waliokulea na kukuza, Mtoto wako ndio huyo tu mmoja uliyenae!! Na unaweza ukapata mume mwingine!!! Kwanini??" Darasa likawa na ukimya wa hali ya juu, kila mmoja akitamani asikie ni nini Cathy atajibu. Cathy kwa ujasiri na utulivu akainuka na kusema, "siku moja wazazi wangu watatangulia kufariki (Mwenyezi Mungu anisamehe), mtoto wangu pia ataondoka pale atakapokua mkubwa kwenda kuanzisha familia yake. Mtu nitakayebaki nae kumaliza nae maisha hasa uzeeni ni mume wangu tu!! Yeye ndiye niliyeunganishwa nae na Mungu, mimi na yeye ni mwili mmoja." Wanafunzi wote wakasimama na kumpigia makofi kwa kushare nao ukweli na msimamo wa maisha yake. Huu ulikuwa uamuzi wa Cathy, yeye kwa mtizamo wake alimchagua mumewe. Je wewe ungechagua nani? Kwa upande wangu bado natafakari

Ijue kwa undani nchi ya BRUNEI

IJUE KWA UNDANI NCHI YA BRUNEI AMBAKO RAIA HAWALIPI KODI 1. Brunei ukipenda iite 'Darusalaam' ama nyumba ya amani ni nchi ambayo raia wake hawalipi kodi yeyote (All citizens in Brunei, including expats, do not have to pay for taxes, for it is absolutely free.), Hata maisha ya wananchi wake ni mazuri na mshahara wa chini kabisa ni dola 25 kwa saa (Tshs 50,000) huku ukosefu wa ajira ukiwa ni wastani wa 5% tu. Serikali inalipa gharama zote muhimu, mpaka chakula kinalipiwa ruzuku. ukifanya kazi kule hakuna income tax (There is no personal income tax or capital gains tax). Sultani anasimamia vizuri sana export ya mafuta na gesi na wanachi wanakula bata watakavyo. GDP ya Brunei imepanda hadi 56% kuwa nchi ya tano duniani (16.11 billion USD in 2013) na IMF wanasema nchi hiyo haidaiwi HATA MIA.... 2. Sultan wa Brunei Mohammad Hassan Bolkiah ndiye Raisi tajiri kuliko maraisi wote duniani, Maarufu kwa utumiaji wa dhahabu kwa kila kitu, hali ila na vijiko vya dhahabu, na nguo anazo vaa zimepambwa kwa dhahabu na fedha. Huyu anamiliki Jumla ya MAGARI 5000 YA KIFAHARI (tazama kasri na moja ya gari lake lake la dhahabu tupu pichani). Sultan huyu anamiliki pia ndege aina ya Boing 747 thamani yake ikiwa ni dola milion 100 ambamo pia nakshi pekee ni dola milioni 120 humo utakuta vyoo na vyumba vya dhahabu, pia anamiliki ndege ndogo sita na helicopta moja. Arusi ya mtoto wa Sultan wa Brunei ilifanyika kwa muda wa siku 14 kwa gharama ya 5 milion dolla huku watu wote walioalikwa wakila na kunywa na kusaza, na kuhudhuriwa na zaidi ya maraisi 25. 3. Elimu ni Bure kabisa na watoto chini ya miaka 12 HUTIBIWA BURE huku watu wazima wakilipia dola 1 tu kwa Matibabu. Kadhalika ukioa tu unapewa na gari. Ni nchi mojawapo ambayo ina uwiano mkubwa wa watu na magari (1:209)-Ikiwa hakuna tiba ya ugonjwa wako Brunei unapelekwa nje ya nchi hasa Malaysia na Singapore kwa gharama za serikali 4. Pombe imepigwa marufuku kabisa kisiwani Brunei ingawa wageni wanaweza kuagiza kiwango chenye ukomo na Hakuna NOA/NGURUWE hata mmoja nchi nzima.................... 5. . Ukiwa Brunei marufuku kupoint kutumia kidole cha shahada kuonesha kitu. Kidole gumba tu hutumika kupoint kitu na ni Lazima kuvua viatu unapoingia nyumba yeyote ndani ya Brunei 6. Hii inatumia mfumo wa SHARIA ambapo 'Wezi hukatwa mikono na wazinifu kupigwa mawe'. Mwaka 2014 ilipitisha sheria ya kupigwa kwa mawe hadi kufa yeyote atakayebainika anafanya USHOGA (Homosexual) lakini kwa uthibitisho wa mashahidi WANNE.....Unaweza kusherehekea Noeli (X-mass) lakini si kwa kuweka mapambo yake kama vilemti wa Xmass nk.......... 7. Ingawa Kisiwa cha Brunei Kina BUNGE lakini nchi hiyo HAINA UCHAGUZI......Uchaguzi wa mwisho ulifanyika mwaka 1962, kuna chombo kimoja tu cha habari kinachomilikiwa na Serikali...ni aghalabu sana kwa media kuipinga serikali 8. 93% YA WATU WOTE WAMEENDA SHULE KWA KIWANGO CHA LAMI (Degree)

Historia ya uhuru wa tz

Ukweli umefichuka, historia ya uhuru wa Tanganyika By. @SANGAPIPI JF Senior Member #1 3 minutes ago Joined: Jun 25, 2013 Kwamujibu wa John Silivalon katika kitabu chake anabainisha nguvu ya kanisa katika siasa ya Tanzania, Lakini John sio yeye tu, @Yericko Nyerere pia katika kitabu chake kiitwacho Ujasisi wa Kidola na Kiuchumi Sura ya Pili, uk 295, ameeleza kwakirefu... Nanukuu "Maamuzi yoyote ya mwelekeo wa dunia hutokea baada ya kukubaliwa ama kuratibiwa na Kanisa kupitia shirika la Jeisuti ambalo utendaji wake ni wa siri zaidi. Karne ya 17 kanisa lilikuja na mpango madhubuti wa kuisaka haki ya kibinadamu katika ulimwengu wa kikoloni, ijapokuwa mpango huo ulikuwa ukibadilika malengo kila nyakati kulingana na mahitaji ya karne. Baada ya vita vya kwanza vya dunia, Shirika la Wajeisuiti lilikuwa na nguvu na lilikuwa tayari sehemu ya tawala nyingi duniani hivyo kufanya kisiwepo kitakachofanyika bila majasusi hawa kujua ama kuhusika, hasa juu ya mstakabali wa dunia ijayo, walikuwa na bado wanauoni mkubwa wa mambo yajayo. Wazo la kuwa na Shirikisho la Mataifa lilitolewa mara ya kwanza na mwanafalsafa Mjerumani Immanuel Kant mnamo mwaka 1795. Wazo la Kant lilirudiwa na wanafalsafa mbalimbali. Wakati wa vita kuu ya kwanza rais wa Marekani Woodrow Wilson alipendekeza hatua za kuanzisha shirikisho hili kwa kusudi la kuzuia vita za wakati ujao baada ya mwisho wa vita ile. Kant alikuwa wakala wa ujasusi wa Wajeisuiti akiripoti kwa Karl Theodor von Dalberg, alizaliwa mjini Königsberg (sasa: Kaliningrad) 22 April 1724 kama mtoto wa fundi. Mamake alimsomesha kweye shule ya sekondari akaendelea kusoma theolojia, falsafa, sayansi, fizikia na hisabati. Tasnifu (thesis) yake ya kwanza haikupokelewa na profesa wake mwaka 1746 hivyo alifanya kazi ya ualimu kwenye nyumba ya matajiri na makabaila mbalimbali kwenye mazingira ya Königsberg. Mwaka 1754 alirudi kwenye chuo kikuu akamaliza masomo yake. Tangu 1755 alikuwa mwalimu na tangu 1870 profesa kamili kwenye chuo kikuu cha Königsberg.Hakuoa aliishi na mtumishi wa nyumbani tu hadi kifo chake mwaka 1804 kwa umri wa miaka 80. Kaburi lake ni kando la kanisa kuu la Königsberg limetunza hata siki hizi baada ya kufukuzwa kwa Wajerumani na kuwa sehemu ya Urusi. Katiba ya shirikisho la mataifa ilikuwa sehemu ya mkataba wa Versailles mwaka 1919. Nchi washindi au mataifa ya ushirikiano zilijiunga na umoja huo mpya. Baada ya kukubaliwa na nchi za kutosha shirikisho lilianza rasmi tarehe 10 Januari 1920.Katiba ilikuwa na madhumuni kama yafuatavo: Fitina zote kati ya nchi zitasuluhishwa kwa njia ya amani kwa azimio ya kamati au mahakama ya kimataifa. Nchi wanachama zote zitaungana dhidi ya nchi yoyote itakayoanzisha vita mpya au kukataa azimio la mahakama ya kimataifa. Nchi zinapatana kupunguza jeshi zao na idadi ya silaha zilizopo Mkutano mkuu wa. Kamati kuu au halmashauri ya nchi wanachama nne (baadaye sita)na nafasi nne (baadaye 9) za nchi zinazobadilishana kwa zamu. Ofisi kuu inayoongozwa na Katibu Mkuu Mahakama ya kimataifa inaundwa ya kutoa azimio katika matatizo kati ya madola. Mkataba wa Versailles ulianzisha aina mpya ya maeneo yaliyowahi kuwa ama koloni au majimbo ya nchi zilizoshindwa katika vita. Koloni zote za Ujerumani pamoja na sehemu kubwa ya majimbo ya Milki ya Osmani ya awali ziliwekwa chini ya mamlaka ya Shirikisho la Mataifa na kukabidhiwa kwa nchi washindi wa vita. Zilipewa hali ya pekee kama maeneo ya kudhaminiwa. Tofauti na koloni za kawaida nchi wadhamini hazikupewa mamlaka yote jinsi iliyokuwa katika koloni zao za kawaida bali zilipokea maeneo ya kudhaminiwa chini ya masharti fulani pamoja na kulinda haki kadhaa za wenyeji na KUZIANDAA nchi hizi kwa uhuru. Hapo mwanzoni tofauti kati ya koloni na eneo la kudhaminiwa haikuwa kubwa lakini baadaye masharti ya udhamini yalikuwa muhimu. Kwa mfano hali ya Tanganyika kuwa eneo ka kudhaminiwa ilisababisha Uingereza kutokubali walowezi wengi kuja hapa. Vivyo hivyo hali ya Afrika ya Kusini Magharibi kuwa eneo la kudhaminiwa ilizuia sehemu hii kuwa jimbo la Afrika Kusini kuwa msingi kwa uhuru wake kama nchi ya Namibia. Jukumu la kuandaa nchi hizo kupata uhuru liliratibiwa na shirika hilo la kijasusi kwa ustadi mkubwa bila baadhi ya makoloni kujua, lakini lilikumbana na kikinza hasa kufuatia mnyumbuliko wa kiimani ndani ya ukristu kufuatia nguvu ya Cambrige (Anglikana), mgogoro huo ulikuzwa kwakuwa Anglikana nao tayari walikuwa wameaandaa taasisi yao waliyoiita Fabian Sociaty maalumu kwaajili ya kuwaandaa vijana wa kiafrika kukabidhiwa nchi zao, Barani Afrika Jeisuiti ilibadili mbinu kwakuwa dola la Kiingereza lilikuwa kikwazo kwa sehemu fulani, haikujikita kwenye dola isipokuwa ilisimama katika muundo wa shirika lifanya shughuli zake ndani ya Kanisa. Dhamiri ilikuwa lazima itimie, kama ilivyosemwna huko mwanzo kuwa hawa ndio wabobevu wa elimu ya juu kwa kila nyanja na ndio wanaotawala ulimwengu, hivyo vikwazo havikukwamisha wao kufikia malengo. Katika Tanganyika chini ya Udhamini wa Jumuiko la Kimataifa, kulikuwa na harakati za hapa na pale za kudai haki za kiraia kwa wenyeji. Ifahamike kuwa vyama vya harakati hizo Tanganyika vilikuwa vingi sana, na vipo vilivyokuwa vikipingana vyenyewe kwa vyenyewe. Mwaka 1927 hadi 1929 kanisa Katoliki nchini chini Joseph Gabriel Zelger, lilibainika kuingiza siasa katika utendaji kazi zake, kitendo hiki kiliwakwaza wakuu wa mamlaka ya kikoloni na kupelekea majasusi wakikoloni wapendekeze aachishwe uongozi wa kanisa nchini. Ni kweli tarehe 12 februari 1929 Zelger alistaafu wadhifawake kwa lazima. Ni mwaka huohuo wa 1927 ndio Chama cha African Assosiotion (AA) kilianzishwa na Gavana Sir David Cameron maaluma kwaajili ya kuratibu sherehe za watu weusi huko pembeni ya mji huko mtaa wa Stanley (leo Lumumba) na kuwapa ofisi mahali leo wanapojiita TANU ilizaliwa. Lakini historia ya Tanganyika haiwataji waasisi wa AA, Rais wa kwanza Mwalimu Cesil Matola (msomi wa mwanzo kabisa enzi za mjerumani kutoka kabila la Wayao), katibu mkuu wa kwanza Klest Sykes (Mzulu Baba yake alikuwa mateka wa kikoloni toka Afrika Kusini), Mwekahazina Ali Ramadhan (mzaramo na mvuvi maarufu wa pwani la Azania). Hao ndio mwaka 1927 waliounda Chama cha kwanza kabisa cha kutetea maslahi ya weusi Tanganyika na shughuli zake zilikuwa ni kuratibu sherehe za waafrika tu. (Chama cha walevi kwa lugha nyingine). Mwaka 1933 Mwalimu Cesil Matola alifariki na nafasi yake ikakaimiwa na katibu mkuu wa chama hicho bwana Klest, mpaka ilipofika mwaka 1948 yakatokea mapinduzi yaliyoongozwa na mtoto wa Klest aliyeitwa Abdulwahid Sykes huyu alikuwa ametoka kupigana vita vya pili vya dunia huko Burma, na aliporudi alikuwa na mawazo ya ujana toka vitani, akampindua baba yake kwa kumpiga ngumi puani, mapinduzi yaliyoitwa “ondoa wazee”. Kisha AA ikabadilishwa jina na kuitwa TAA, Rais wake wa Kwanza akawa Dr Vedasto Kyaruzi (Mhaya), huyu ndie dakitari wa binadamu wa kwanza kabisa wa kiafrika Tanganyika, Katibu mkuu akawa Abdulwahid Sykes na Mweka hazina akawa Dosa Azizi, utawala huo ulienda mpaka mwaka 1953 uchaguzi ulipofanyika na Nyerere akashinda pale kwenye ukumbi wa Anautoglo Mnazimoja leo, mwaka 1954 Nyerere akabadili jina la chama na kuwa TANU jina ambalo lilibuniwa na Abdulwahid Sykes, TANU ilikwenda mpaka mwaka 1977 na kisha kikazaliwa chama kiitwacho CCM baada ya Muungano wa ASP na TANU. Kisa hiki cha kufukuzwa kwa Kasisi huyu Bw. Zelger kinasema, Kanisa lilianzisha mafundisho yenye kuchochea fikra za kimaasi, nalilifanikiwa kuandaa wakufunzi maalumu kwenda katika majimbo yote ya kihuduma Tanganyika, hilo lilipelekea kuleta mtafaruku na dola ya mkoloni wa kiingereza ambapo ilimgharimu kiongozi huyu wa kiroho kuachia madaraka yake. Alipoingia askofu Edger Aristide Maranta mwaka 1930, ikiwa kama vile mwendelezo wa mtangulizi wake, Askofu Maranda alianzisha harakati za kuwashawishi viongozi wengine wa majimbo kuendeleza kutoa mafundisho yenye kumfanya mtanganyika ajitambue na adai uhuru wake, mfano, 23 mei 1938 wakati makanisa saba ya Kilutheri yakiwa kwenye hatua za mwanzo za mchakato wa kuungana, Askofu maranda aliomba kuhudhuria kikao cha tarehe 8 mwezi wa sita kilichofanyika Mjini Arusha, Askofu Maranda aliudokeza mpango ule wa siri wa katoliki katika kikao hicho, japokuwa kulikuwa na hofu ya kutoaminiana, lakini uthabiti wa malengo hayo ulijipembua baadae na kuwa wamafaa, ushahidi wa nyaraka za kumbukumbu za mkutano huo unaeleza. Juhudi za kanisa kupigania mkataba wa Versailles ziliendelea kushika kasi huku zikiendeshwa kwa siri sana kwamfumo wa neno la kiroho, na ilipofikia miaka ya 1950+ kanisa sasa lilikuwa tayari linanguvu ya ushawishi kufuatia mafanikio ya harakati za kanisa katika nyanja za ukombozi barani afrika. Wakati hayo yakiendelea tayari kanisa kupitia shirika lake la kijasusi lilikuwa limewekeza kwa nguvu kubwa kumtafuta mtu imara mwenye weledi na vipawa atakayejengwa ili aje kuongoza nchi. Mtihani mkubwa kwa kanisa ilikuwa ni namna gani linaweza kuingia rasmi kudai uhuru wa Tanganyika. Katika kipindi hiki tangu harakati za kanisa zianze, Askofu Maranta pamoja na mapadre wa baadhi ya mikoa, walikuwa tayari ameshafanya juhudi kadhaa za kukutana na Mashehe waliokuwa na ushawishi mkubwa, mfano 05/02/1948, Askofu Maranda alikutana Shehe Issa bin Amir kiongozi wa kiroho katika msikiti wa Ilala - mchikichini. Shehe Issa Bin Amir alizaliwa 1846 katika viunga vya Mzizima, mchikichini na kuhudumu katika wadhifa wa shekhe katika msikiti uliokuwa hapohapo viwanja vya nyumbani kwake na alifariki mwaka 1953 akiwa na umri 107, Shehe Issa Bin Amir kwa kabila alikuwa Mzaramo na akiishi hadi kifo chake Mchikichini pale nyuma ya kilipo kiwanda cha bia leo (TBL). Shehe Issa Bin Amir rafiki kipenzi wa Padre Maranta na mzee wa hekima za kilele cha zama hizo, mtu aliyekuwa kiungo muhimu kati ya uislamu na ukristu, Mtu ambae Mwalimu Cesil Matola rais wa kwanza wa AA na Klest Sykes katibu mkuu wakwanza wa AA, na wanachama wengine waliokuwa AA walimheshimu sana kwa hekima zake na mmoja wa wasisi wa Jumuiko la Uislamu Afrika Mashariki (EAMWS) Mazungumzo yao yalihusu harakati za ukombozi, Shehe Issa alimshauri Askofu kuwa ikiwa makanisa na misikiti yanapigwa marufuku na mkoloni kujihusisha na siasa za ukombozi basi watafute baadhi ya vyama vya harakati za ukombozi na waviunge mkono, wazo hilo lilimvutia Askofu lakini akajenga hofu kama je ndani ya vyama hivyo watapata vijana wasomi?. Siku chache baada ya makutano yake na Shehe Issa, Askofu Maranta aliletewa mapendekezo kutoka kwa Attilio Beltramino kasisi wa katoliki aliyehudumu kule Iringa, mapendekezo ya kasisi huyu yalikuwa ni, Umishonari makao makuu uruhusu udurufu wa biblia zisomeke kwa makabila ya wahusika wa eneo, ndani ya biblia hizo yaongezwe mafundisho ya haki ya kujitambua na kujitawala wenyewe. Pendekezo hili lilimvutia sana Maranta hivyo akalipa baraka zake, kwa hakika lilifanikiwa na ndio lilizaa hisia kali za mwamko wa kudai uhuru, mfano biblia ya lugha ya kihehe ilikuwa inaeleza wazi athari za kutawaliwa. Harakati za Ukombozi za Mwalimu Nyerere akiwa na nguvu mpya ya kifikra toka Chuo kikuu, zililivutia kanisa na uungaji mkono ukachagizwa, mfano mwaka 1953 wakati TAA kikiwa chama chenye nguvu kufuatia mabadiliko ya 1948 toka AA kwenda TAA. Askofu Maranta alimwalika ofisini kwake Mwalimu Nyerere, walizungumza mengi lakini kubwa nikuwa alimsifu kwa juhudi za kujipambanua bila kuwaogopa wakoloni, akamweleza jinsi kanisa linavyounga mkono juhudi za ukombozi wa Tanganyika, kisha akamshauri kuwa ajaribu kuvishawishi baadhi ya vyama vya harakati za kiraia viungane ili kuvipa nguvu ya kudai uhuru na kanisa litasaidia. Wazo la Askofu Maranta lilimkaa Mwalimu Nyerere na mwaka 1954, alianza juhudi za kuwaunganisha vijana wenzake wa kariakoo ambao walikuwa ndani ya TAA na wenye nguvu ya ushawishi lakini wakikabiliwa na matatizo makubwa mawili katika lengo lao ambayo ni Elimu na Woga. Ikumbukwe kuwa mwaka 1953 baada ya harakati za ukombozi kupamba moto na kamata kamata ya wanaukombozi, Askofu Edger Aristide Maranta alihamishiwa Zanzibar na nafasi yake ikachukuliwa na Vicar Apostolic, lakini bado aliendelea kuwa mshauri imara wa Mwalimu Nyerere. Jambo la kushangaza kama si kufurahisha, mwaka huohuo mwezi wa 8, Edger Aristide Maranta alirudishwa tena Dar es Saalam, na sasa mbinyo dhidi ya ukoloni ukashika mkondo wake. Mnamo tarehe 07/07/1954, Vijana (wazee wa kariakoo) wakiongozwa na Julius Kambarage Nyerere, walikubaliana wazo la kuhuisha chama kutoka TAA kwenda TANU, chini ya uratibu wa karibu wa Wajeisut (Askofu Maranta) na Waislamu (Shehe Issa bin Amir) ijapokuwa alikuwa amefariki mwaka mmoja nyuma, lakini hekima za Shehe huyu zilisaidia. Na zaidi ni kuwa safari ya kwanza ya Mwalimu Nyerere ya kwenda UNO 05/03/1955 Kanisa Katoliki lilitoa msaada kwa chama cha TANU wa tiketi ya ndege ya kwenda na kurudi, lilifanya hivyo kupitia shirika lake la Maryknoll Sisters la New York Marekani, Si hivyo tu bali katika moja ya utani wa Mwalimu wenye ukweli ndani yake aliwahi kusema kuwa makasisi Walsh na Art Wille wa Shirika la Maryknoll ni maboss wake, akikumbuka malipo ya shilingi 600 angali ameacha kazi ya ualimu akiwa kijijini Butiama.Kuna ushahidi wa kihistoria pia unaochagiza habari hizi kwamba majasusi wa Kanisa walimuandaa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuja kuwa kiongoza Tanganyika mpya. Barua ya lugha ya kilantini ya kitume TOT TANGAEQUE ya 8 Novemba 1984 ya Papa wa Roma kwenda kwa Kanisa la Katoliki Tanzania inautangazia ulimwengu kwamba Tanzania itakuwa chini ya himaya ya kanisa kwa mwavuli wa Bikira Maria Imakulata." NB Nashukuru sana kuona watu wanasoma na kuthamini kazi yangu nakuitumia kama rejea katika maandishi yao....

Monday, 5 December 2016

JE UNAKUMBUKA?

1. Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali, Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili, Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali, Wakataka na kauli iwafae maishani. 2. Akatamka mgonjwa, ninaumwa kwelikweli, Hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali, Roho naona yachinjwa, kifo kimenikabili, Semeni niseme nini, kiwafae maishani. 3. Yakawatoka kinywani, maneno yenye akili, Baba yetu wa thamani, sisi tunataka mali, Urithi tunatamani, mali yetu ya halali, Sema iko wapi mali, itufae maishani 4. Baba aliye kufani, akajibu lile swali, Ninakufa maskini, baba yenu sina hali, Neno moja lishikeni, kama mnataka mali, Kama mnataka mali, mtayapata shambani. 5. Wakazidi kumchimba, baba mwenye homa kali, Baba yetu watufumba, hatujui fumbo hili, akili zetu nyembamba, hazijajua methali, Kama tunataka mali, tutapataje shambani? 6. Kwanza shirikianeni, nawapa hiyo kauli, Fanyeni kazi shambani, mwisho mtapata mali, haya sasa buriani, kifo kimeniwasili, Kama mnataka mali, mtayapata shambani. 7. Alipokwisha kutaja, fumbo hili la akili, Mauti nayo yakaja, roho ikaacha mwili, Na watoto kwa umoja, wakakumbuka kauli, Kama mnataka mali, mtayapata shambani. 8. Fumbo wakatafakari, watoto wale wawili, wakakata na shauri, baada ya siku mbili, wote wakawa tayari, pori nene kukabili, Kama mnataka mali, mtayapata shambani. 9. Wakazipanda shambani, mbegu nyingi mbalimbali, tangu zile za mibuni, hadi zitupazo wali, na mvua ikaja chini, wakaona na dalili, Kama mnataka mali, mtayapata shambani. 10. Shamba wakapalilia, bila kupata ajali, Mavuno yakawajia, wakafaidi ugali, Wote wakashangilia, wakakumbuka kauli, Kama mnataka mali, mtayapata shambani. 11. Wakanunua na ng'ombe, majike kwa mafahali, wakapata na vikombe, mashine na baiskeli, Hawakuitaka pombe, sababu pombe si mali, Kama mnataka mali, mtayapata shambani. 12. Wakaongeza mazao, na nyumba za matofali, Pale penye shamba lao, wakaihubiri mali, Wakakiweka kibao, wakaandika kauli... "KAMA MNATAKA MALI MTAIPATA SHAMBANI". 🚶🚶🚶🚶🚶🚶 Miaka hiyo tuliimba tu kama kujifurahisha wala hatukujua maana yake, leo twatambua nini maana yake, nasisitiza, kama mnataka mali mtaipata shambani *MAANA MSEMO WA ELIMU NDIO UFUNGUO WA MAISHA HAUNA DILI TENA KWA HALI ILIVYO*

UNGEKUA WEWE UNGEFANYAJE

UNGEFANYA NINI? Mwanamke alimkimbia mumewe na akamuachia mtoto mwenye miaka mitatu. Sababu kubwa ya kumkimbia mumewe ni kwamba alipata boyfriend mwenye hela ambaye alikuwa akiishi Michigan huko Marekani. Huyo Boyfriend au mchepuko wake walijuana kupitia mitandao ya kijamii. Walizoeana sana na mwisho yule boyfriend wake akamuahidi kumtafutia viza ya kuishi Marekani. Na kweli baada ya miezi kadhaa yule mwanamke alimtoroka mumewe na kutokomea Marekani, huku akiacha taarifa kwamba asitafutwe tena, anaenda kuanza maisha mengine mapya. (mumewe alifirisiwa kutokana na kutuhumiwa ubadhirifu wa mali za kampuni alikokuwa akifanya kazi). Kutokana na msongo wa mawazo na upweke kwa kipindi kirefu tokea mkewe amtoroke, yule mwanaume akaamua kuoa mke mwingine. Kwa bahati mbaya yule mwanamke mwingine aliyeolewa hakuweza kushika mimba. Hata hivyo yule mwanamke mwingine alimtunza vema mtoto wake wa kambo kama mwanae vile. Miaka michache baadae, yule mume alifariki kwa ajali ya gari alilokuwa akisafiri nalo kwenda kijijini kufanya biashara ya mazao. Mke wake wa pili alifanya kila jitihada kwa uwezo wale wote kumsomesha yule mtoto, na Mungu hakunyimi vyote kwani yule mtoto alikuwa na uwezo mkubwa wa kiakili. Mwanamke aliuza nyanya sokoni, alitembeza ndizi, alichoma mahindi barabarani na kadharika ilimradi aweze kujitunza yeye na yule mtoto wake wa kufikia. Yule mtoto alijua kwamba yule ndiye mama yake halisi na ndiye aliyekuwa akimuita mama. Mama yake halisi aliyetorokea Michigani, Marekani, hakuwahi hata siku moja kutuma salamu au kuwasiliana na mtoto wake, ingawa alipata habari kwamba mumewe wa zamani alifariki kwa ajali. Miaka mingi ilisonga na kijana alikuwa kwa akili na kimo, alikuwa Chuo kikuu akisomea Uhandisi wa mafuta na gesi (Bachelor of science in petroleum Engineering). Mama yake halisi aliyeko Marekani hakuweza kupata mtoto tena na yule mwanaume mwingine aliyemuoa, na kwa hilo yule mume wake mpya aliamua kumtimulia mbali. Kwa kutambua kuwa alifanya kosa kumkimbia mwanae, aliamua kurudi nyumbani kumtafuta mwanae na kumkabidhi utajiri alioupata akiwa Marekani (gawiwo la nusu kwa nusu la mali baada ya kutalikiana na mumewe wa Marekani) Bahati mbaya alifika na kumkuta mwane akipigania kati ya uhai na kifo kutokana na kufeli kwa figo zake. Madaktari walikuwa wakihitaji pesa nyingi kwa ajili ya upasuaji, pesa ambazo mama yake wa kambo alishindwa kabisa kuzipata. Mama yake halisi kutoka Marekani aliingilia hilo suala na kulipa pesa zote za hospitali kwa ajili ya matibabu, pia akatoa figo yake moja na maisha ya kijana yakawa yameokolewa. Baada ya matokeo ya mwisho ya chuo kikuu kutoka, kijana alipata ufaulu wa hali ya juu (first class degree) na akapewa ufadhili wa kwenda kusomea shahada ya uzamivu (masters) na baada ya hapo udaktari wa falsafa (phd) huko Burnley, Uingereza. Katika kupokea cheti chake siku ya mahafali chuoni kwao, makamu mkuu wa chuo alimpa kipaza sauti kijana na kumwambia amuite mama yake katika stage na kupokea cheti cha heshima. Baada ya makamu mkuu wa chuo kusema hayo, mama yake halisi aliyemkimbia alisimama na kujiweka sawa kusubiri kuitwa na mwanae, wakati mama yake wa kambo aliyemlea tokea mdogo akiwa bado amekaa huku machozi mengi yakimtoka huku akimuangalia mwanae wa kufikia kule mbele. Jibu naliacha hewani......................... Fikiria wewe ndio huyo mtoto, utamuita nani aje kule stejini kupokea hicho cheti? A) Mama wa kambo B) Mama mzazi Nahitaji majibu yenu, kama huna share kwa wengine waje na majibu.

Sunday, 23 October 2016

Mbinu 5 za kukunufaisha maishani

Mbinu 5 za kukufanikisha maishani Unaweza ukawa upo kwenye hali ya kulalamika maisha yako ni magumu na unashangaa kwa nini hufanikiwi katika maisha yako kama jinsi unavyotaka wewe. Hali hii inaweza ikawa inakuumiza pengine kila ukiangalia rafiki zako ama maisha ya wengine yanavyozidi kuwa mazuri, wakati wewe upo katika hali ngumu. Na pengine umekuwa ukijiuliza nini siri kubwa ya mafanikio yao ambayo wanaitumia ambayo wewe huna. Kutokana na hali hiyo umekuwa ukijilaumu kujilaumu na kujiuliza kwanini nyingi ambazo hazina majibu. Kitu usichokijua watu hawa huwa wanatumia mbinu fulani kufanikiwa. Kawaida, katika maisha kama ulivyomchezo wa miguu, au michezo mingine mara nyingi huwa zipo mbinu za kufanikisha kile tunachokifanya. Mbinu hizi huweza kutambulika kama sheria, kanuni, au siri lakini zote hulenga kukufanikisha kama unataka mafanikio ya kweli. Mbinu hizi zinapotumiwa kwa bahati mbaya au nzuri huwa hazifanyi ubaguzi zinamwendea yoyote na kuleta matunda unayoyataka. Hata kama ikitokea umezitumia mbinu hizi kwa bahati mbaya bila kujijua ni lazima utafanikiwa katika maisha yako. Mbinu hizi ndizo wanazozitumia wengi wenye mafanikio na kuwafanikisha, ingawa huwa sio kwao kuwa rahisi kukwambia mbinu hizo. Haijalishi unaishi kwa sasa maisha gani au upo kwenye matatizo mengi vipi, ukizitumia mbinu hizi, zitakufanikisha na kukupa maisha ya mafanikio unayoyataka. Acha kulalamika tena na kuishi bila amani. Sasa unaweza ukawa na mafanikio makubwa kama hao unaowaona wamefanikiwa, ikiwa utatumia mbinu hizi kukufanikisha. Unajua mbinu hizi ni mbinu zipi? Hizo Ndizo Mbinu 5 Za Kukupa Maisha Ya Mafanikio:- 1. Kuwa na nidhamu binafsi. Ili kupata mafanikio makubwa unayoyahitaji sio suala la kufanya kazi kwa bidii tu, zaidi unachohitaji nikuwa na nidhamu binafsi ambayo itakuongoza kwenye malengo yako. Watu wengi hawana nidhamu binafsi kitu ambacho kinapelekea wengi ndoto zao zinaishia kati. Ni muhimu kuelewa kuwa ni lazima kufanya mambo yale yanayoendana na ndoto zako, hata kama kuna wakati unajihisi umechoka unalazimika kujikaza kufanya jambo hata dogo ambalo litakufikisha kwenye malengo yako. Ukishindwa kuwa na nidhamu binasi katk maisha yako elewa kuwa utashindwa kufikia mipango na malengo iliyo jiwekea. 2. Jifunze kila mara kwa watu waliofanikiwa. Hii itakusaidia kujua vitu vingi usivovijua kuliko kukaa na kung’anga’nia mbinu zilezile ambazo hazikusaidii. Yapo mambo mengi sana usiyoyajua ambayo yanakufanya ushindwe kufanikiwa. Ikiwa utakuwa na uwezo wa kujifunza kwa wale waliofnikiwa utakuwa upo kwenye nafasi kubwa ya kufanikiwa na kusonga mbele. Maisha yako yanazidi kuwa magumu siku hadi siku, kutokana na kukosa kujifunza kwa wengine kwa kujua hilo badili mwelekeo wako na kuwa mtu wa kujifinza mwisho wa siku mafanikio yatakuwa makubwa kwako. 3. Jifunze kutokana na makosa uliyofanya. Inawezekana kuna mahali utakuwa umekosea kwa namna moja au nyingine,badala ya kulaumu na kuumia moyo sana jifunze kutokana na hayo makosa liyoafanya ili isije ikawa kwako rahisi kufanya makosa yaleyale kwa mara nyingine. Ikiwa utajifunza kutokana na makosa na kufanyia kazi kile ulichojifunza hapo utakuwa umechukua hatua moja muhimu ya kuweza kukusaidia kusonga mbele kuyafata mafanikio unayoyataka. Unataka mabadiliko makubwa katika maisha jifunze kutokana na makosa yako na acha sana kulaumu. 4. Jenga tabia ya kujisomea kila siku. Hili ni jambo ambalo nimekuwa nikiliongelea sana kuhusu huu umuhimu wa kujisomea. Unapojisomea unapata vitu vingi sana tena ndani ya muda mfupi. Kupitia huko utaweza kujifunza mambo mazuri yatakayoweza kubadili maisha yako kwa sehemu kubwa na kuwa mtu, tofauti kabisa. Acha uvivu jifunze vitu vipya kila siku. Unaweza ukajifunza kupitia vitabu, ama mitandao mizuri inayoelimisha kama huu wa DIRA YA MAFANIKIO kwa kupata maarifa bora na sahihi kabisa. Unapojifunza inakusaidia kukabiliana na changamoto nyingi, ambapo kwako ingekuwa ngumu kuzikabili. 5. Kuwa na mahusiano sahihi na watu waliofanikiwa. Katika kutafuta mafanikio ni vizuri ukawa na mahusiano ama mtandao na watu sahihi ambao watakusaidia kukufikisha kwenye lengo ulilojiwekea. Haina haja kuwa na watu ambao hawakusaidii kutimiza malengo yako. Watu hawa watakukwamisha na kukurudisha nyuma katika maisha yako tu siku zote. Jenga tabia ya kuwa na watu sahihi ambao utajifunza kitu kwao, utashirikiana nao na kujifunza mambo mengi huko ya mafanikio na hatimaye utamudu kusonga mbele

Virefu vya majina ya vijiji vyetu Kilimanjaro

WELCOME TO K'NJARO OUR HOMELAND! Angalia virefu vya majina ya vijiji vyetu. MOSHI=Mungu Onyesha Sehemu Hela Ilipo; ROMBO=Ruhusu Ongezeko la Mapesa Bila Ombaomba; HIMO=Hata Ikipungua Mungu Ongeza; MARANGU=Mungu Angalia Raia Ngawira Utuhakikishie; MAMBA=Mungu Ahidi Mapesa Bila Ajira; MWIKA=Mungu Wekeza Ishara Kwenye Akaunti; URU=Usitunyime Riziki Uchumi; KIBOSHO=Kila Ikipungua Baba Ondoa Siasa Hela Ongeza; MACHAME=Mungu Atupe Chanzo Halisi na Ambacho Mapesa ni Endelevu na KISHIMUNDU=Kwetu Ikikosekana Shilingi Mungu Nakuapia Dunia Utaichukia! Rusha sms hii kwa wachagga wote *waambie tunasaka mahela na hatupendi ujinga sisi*😎😎😎

Kama mwanamke una tabia hiz utazeekea nyumbani

*KUOLEWA NI NDOTO KUU YA KILA MWANAMKE ALIYEKAMILIKA ILA KAMA UNA TABIA HIZI UTAZEEKEA NYUMBANI* 1. Tamaa ya utajiri, fedha na mali nyingi pasipo kutambua kuwa vitu hutafutwa. Hapa wengi hupoteza nyota zao kwa kuwakataa wanaume wenye kipato cha kawaida na kujirahisisha kwa wenye nazo ambao kwa bahati mbaya wengi wao sio waoaji bali ni wahuni tu na watu wa anasa na kula bata mjini. 2. Dharau, maringo, kiburi na mashauzi classic. Yaani we kila mtu akikusogelea na kujaribu kuzungumza na wewe unaanza kumpandisha na kumshusha kisha unamsonya. Wengi huishia kukupotezea wakijua labda umewadharau au tayari una mtu wako ndio maana una nyodo nyingi. 3. Huna Jumapili wala Ijumaa, yaani huendi kanisani wala msikitini, husali wala humuombi Mungu hakika lazima wahuni watapata nafasi kwako na kukuchezea mpaka uchakae kama mitumba wa ya mnadani. MUNGU NI NGUZO KUU YA BARAKA ZAKO ukimuomba hakika atakuepushia kuingia midomoni mwa dubu na fisi wanaokuvizia na kuja kama malaika. Atakupa ufahamu wa kuwatambua na kuwashtukia mapema. 4. Kuvaa nguo za ajabuajabu kama changudoa. Sijui ni nani aliyewaambia kuwa mkivaa hivyo mnapendeza! Unakuta binti kavaa kama mcheza show za night club, yaani akipita nguo inaonesha kila kitu na akiinama ndio balaa kabisa yaani kimini kinafunua kila kitu nje nje. Kwa staili hiyo nani atakupeleka kwao? 5. Kujipaka mirangi ya ajabuajabu usoni kama mwali wa kimakonde au kizaramo eti wenyewe mnaziita make-ups. Kwanza mnatutisha tu. 6. Kupenda kujirahisisha au kujipendekezapendekeza kwa wanaume, yani ukiguswa kidogo tu twende. 7. Kuwa na picha karibia 500 Facebook, Twitter, Whatsapp n.k halafu picha zenyewe hazieleweki yaani umepigwa katika mavazi au mapozi ya ajabuajabu, mara umebinua makalio, mara tumbo, mara mdomo, Haaaaa! 8. Kila unachofanya basi unakimbilia kupost. Mfano kwenye Facebook yako au Instagram na nyinginezo hata ukienda haja basi lazima upost. 9. Ni mtu wa manenomaneno yu. Yaani we kila unachokiona unakiongea na kuropokaropoka tu hauna breki, mwanamke gani? 10. Huna mawazo ya malengo endelevu. Yaani we kwenye bichwa lako kumejaa umbea tu sijui leo Wema Sepetu kafanya nini? Sijui Kim, Rihanna, Adelle wamefanya vile na upuuzi mwingine. 11 Mizinga. Yani siku ya pili tu baada ya kukutongoza unaanza "Baby nataka Samsung Galaxy, mara iPhone 7, mara baby nimeona nguo nzuri, mara ooh! baby yaani njaa inauma......kwa hayo mtaishia kusindikiza harusi za wenzio hadi upigwe alama. Waswahili husema, "Kama mzuri, olewa" Jihadhari na tabia hizi. *Nawatakia asubuhi*

Sunday, 9 October 2016

Jinsi ya kujipa msaada ukipata shambulio la moyo

Tafadhali chukua walau dk 2 kusoma hii: 1. Chukulia ni muda wa saa 1:25 jion unarudi nyumbani peke yako, baada ya kazi ngumu zusizo za kawaida ofisini. 2. Umechoka sana, una hasira na umechanganikiwa. 3. Ghafla unajisikia maumivu makali kifuani yanaelekea mkononi na hata kwenye Taya. Upo umbali wa kama km5 tu kufika Hospitali iliyo karibu na kwako. 4. Bahati mbaya hujui kama utaweza kufika kwa unavyojisikia. 5. Ulishafundishwa kumfanyia mtu CPR, lkn aliyekufundisha hakuwaambia unaweza kujifanyia mwenyewe. 6. JINSI YA KIJISAIDIA UNAPOPATWA NA SHAMBULIO LA MOYO UKIWA PEKE YAKO. Kwa kuwa watu wengi hupatwa na Shambulio la Moyo wakiwa peke yao bila msaada wowote, mtu ambaye mapigo yake ya Moyo hayako sawa na anaanza kuhisi kuzimia, au zimebaki sekunde 10 tu kabla hajapoteza fahamu. 7. Hata hivyo, waathirika hawa wanaweza kujisaidia kwa kujikoholesha mfululizo. Avute pumzi ndefu kila anapojikoholesha, na kikohozi lazima kiwe cha ndani mfululizo mpaka makohozi yatoke ndani ya kifua. Kikohozi hicho kiendelee mpaka utakapopata msaada au mpaka mapigo ya Moyo yarudi kawaida tena. 8. Pumzi ndefu hupeleka Oksijeni mapafuni na kikohozi kuubana Moyo na kufanya mzunguko wa Damu uendelee. Nguvu ya kikohozi ya kuubana Moyo pia inasaidia kurudisha ktk mapigo ya kawaida. Kwa njia hii, waathirika wa shambulio la Moyo wanaweza kufika Hospitali. 9. Sambaza ujumbe huu kwa watu wengi uwezavyo, utakuwa umewasaidia kuokoa maisha yao!! 10. Mtaalamu amesema, kila anayepata ujumbe huu na akautuma kwa walau watu 10, tunaweza kuwa tumeokoa maisha ya mtu mmoja. 11. Badala ya kutuma vibonzo, sambaza ujumbe huu ambao unaweza kuokoa maisha ya mtu... 12. Kama ujumbe huu utarudi kwako zaidi ya mara moja, usikasirike! Furahi kwa kutambua kumbe watu wengi wanaokujali. Kutoka kwa: Dr. FC Penal (Cardiologist)

Tuesday, 4 October 2016

Kuhusu kabila la wachaga (mangi)

WAJUE WACHAGA Kabila la Wachaga linafahamika kwa wengi kuwa linapatikana mkoani Kilimanjaro. Kwa asili, Wachaga ni mchanganyiko wa Wamasai, Wasambaa, Wataita, Wakamba na Wakahe. Wachaga walianza kuhamia kwenye miteremko ya Mlima Kilimanjaro kwenye karne ya 17. Walipofika wakiwa katika vikundi vidogovidogo waliwakuta wakazi, wenyeji kwenye Misitu ya Mlima Kilimanjaro walioitwa Wakonyingo. Wenyeji hawa ambao huitwa Mbilikimo hawakupenda kuchanganyika na wahamiaji wageni, hivyo wakahama na kuanzisha makao yao ya kudumu kwenye misitu minene iliyopo nchini Kongo. Wachagga ni kabila la watu wenye asili ya Kibantu lakini pia mchanganyiko wa damu, hasa ya Kikushi wanaoishi kaskazini mwa Tanzania chini ya mlima Kilimanjaro, mkoani Kilimanjaro.Shughuli kubwa ya Wachagga ni biashara na kilimo.Wachagga ni kabila la tatu kwa ukubwa nchini Tanzania. Takwimu za mwaka 2003 zinaonyesha kuwa idadi ya Wachagga 2,000,000. Vikundi vya Wachagga Wachagga wana historia ndefu ya asili yao na ya maingiliano yao na makabila mengine. Kabila la Kichagga ni mkusanyiko wa makabila madogomadogo (ya Kichagga) yaliyosambaa kijiografia kuzunguka mlima Kilimanjaro kuanzia mashariki (Tarakea, Rombo) hadi magharibi kwa Kilimanjaro (Siha, Machame). Makabila ya Kichagga ni Wa-Rombo, Wa-Vunjo ambao wanajumuisha watu wa Mwika, Mamba, Marangu, Kilema na Kirua ambayo ndio inajulikana na wengi kama Kirua Vunjo. Ukipenda unaweza kuwagawa watu hawa wa Vunjo kama Wa-Mwika, Wa-Mamba ,Wa-Marangu,Wa-Kilema,na Wakirua.Makabila mengine ni Wa-Old Moshi, Wa-Kibosho, na Wa-Machame, Wa-Uru, na Wa-Siha. Watu wengi wanafikiria kwamba Wachaga wanatokana na asili moja. Ukweli ni kwamba wamegawanyika katika himaya 15, wanatofautiana kwa lafudhi, lugha, rangi na mwonekano wa miili yao. Wachaga wapo katika makundi makuu matatu ya Hai, Vunjo na Rombo. Wale wanaopatikana eneo la Hai ni Wasiha, Wamasama, Wamachame,Wangíuni, Wakibosho, Wauru na Wamoshi. Kwa wale wanaopatikana eneo la Vunjo ni Wakirua, Wakilema, Wamarangu, Wamamba na Wamwika. Kutoka eneo la Rombo ni Wamkuu, Wamashati na Wasseri. Hadi sasa haijulikani vizuri asili ya jina Wachaga, ila wanahistoria wanaeleza kwamba jina hilo linatokana na neno la Kiswahili linaloitwa 'Kichaka'. Inaelezwa kwamba misafara ya wafanyabiashara iliyokuwa ikiongozwa na Waswahili pamoja na Waarabu, walipokuwa wakipita maeneo ya Vunjo waliwaona wenyeji wa huko wakiwa wamejenga vibanda vya kulinda mazao yao yasiliwe na wanyama waharibifu. Wakawaita wenyeji hawa kwamba wanaishi vichakani na kuanzia hapo wageni wafanyabiashara na Wamisionari walipokuwa wanakuja Kilimanjaro walielekezwa na waongozaji misafara yao kwamba wanakwenda kwenye nchi ya “Uchakani”, wakimaanisha kwamba kwa watu wanaoishi vichakani. Hatimaye wageni wakashindwa kulitamka vizuri neno hili na kuliita ìUchagani, Jina hili likawekwa kwenye ramani na kuitwa nchi ya “Wachaga”. Hivyo ndivyo wenyeji waliokuwa wakiishi kwenye Miteremko ya Mlima Kilimanjaro walivyopewa jina lao. Wachaga. Maendeleo ya Wachaga Maendeleo yao hapo awali yalitokana na zao la kahawa. Walifanikiwa kuanzisha vyama vya ushirika na hatimaye mwaka 1932 walianzisha Halmashauri ya Wachaga (Chaga Council) ambayo kwa sasa inatumiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Moshi. Halmashauri hii iliongozwa na Mangi Mkuu Mshumbue Thomas Marealle II. Mwaka 1946, utawala wa Waingereza uliboresha Baraza la Halmashauri ya Wachaga. Himaya ndogo za Wachaga zipatazo 17 (himaya mbili za Wakahe na Waarusha chini zilijumuishwa kwenye Tarafa ya Vunjo) na kuundwa kwa Tarafa tatu za Hai, Vunjo na Rombo. Halmashauri ya Wachaga ilijenga miundombinu na huduma za jamii ikiwamo kuwasomesha watoto wao kwenye shule na vyuo mbalimbali kama Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda. Halmashauri ya Uchaga ilikuwa na bendera yake ambayo ipo hadi leo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, yenye nembo tano kuu: 1. Mlima Kilimanjaro uliochorwa katikati ya bendera ukionyesha mandhari nzuri ya kilele cha Kibo. Kilele cha Kibo kinatoa maji safi na ni kielelezo cha umoja wao. 2. Chini ya kilele cha Kibo, upande wa kushoto wa bendera kuna mgomba wenye ndizi. Hiki ni chakula kikuu cha Wachaga. 3. Upande wa kulia wa bendera ni tawi la mbuni ukiwa na matunda yake. Kahawa ni zao lililowaletea maendeleo. 4. Bendera imezungukwa na matawi ya 'sale' lenye matawi mawili (draceana plant). Matawi haya yamefanya mduara kuzunguka kilele cha Kibo, mgomba wa ndizi na tawi la zao la kahawa. Masale ni mmea unaoheshimiwa sana na Wachaga wote. Ni alama ya amani. Masale hutumika katika sherehe na shughuli zote za kimila zinazofanywa na Wachaga. Majani yake ni kijani kibichi yanayoonyesha jinsi Kilimanjaro ilivyo na rutuba nzuri inayostawisha mazao ya kila aina. 5. Juu kidogo ya kilele cha Kibo yupo chui ambaye amejipumzisha. Chui ni alama kuu ya mamlaka ya Wachaga. Hapo awali kwenye miteremko ya Mlima Kilimanjaro walikuwepo chui wengi wa rangi nyeusi lakini kutokana na ongezeko la watu pamoja na uharibifu wa mazingira chui hawa wametoweka. Sikukuu ya Wachaga Sikukuu ya Wachaga wote ilikuwa ikiadhimishwa Novemba 10 kila mwaka kama kumbukumbu ya siku ambayo Wachaga wote walipokusanyika na kumchagua Mangi Mkuu baada ya kuteuliwa na Halmashauri Kuu ya Uchaga. Maadhimisho ya kwanza ya mwaka 1952 yalitanguliwa na uchaguzi wa Halmashauri ya Wachaga wote kuanzia kwenye ngazi ya Uchili (kijiji), Umangi ( uchifu wa eneo) na mwisho ngazi ya baraza kuu. WAJUE WACHAGGA Lugha ya Kichagga Lugha ya Kichagga inabadilika kuanzia unapotoka Tarakea mpaka unapofika Siha magharibi mwa Kilimanjaro. Kutokana na tofauti hizo Kichagga kimegawanyika katika Kirombo, Kivunjo, Ki-Old Moshi, Kiuru,Kikibosho, Kimachame, na Kisiha. Lugha hizo zinakaribia kufanana kadiri makabila hayo yalivyopakana. Kwa mfano, Kivunjo kinafanana na Ki-Old Moshi. Vile vile Kisiha kinafanana sana na Kimachame ambacho pia kinafanana kidogo na Kikibosho. Baadhi ya Wamachame walihamia sehemu za Meru, Arusha, na kuchanganyikana na Waarusha, lugha yao ikabadilika kidogo na kuwa Kimeru. Kwa sababu hiyo Wameru wanasikilizana sana na Wamachame ingawa lafudhi zao zinatofautiana kidogo. Historia ya elimu kati ya Wachagga Wachagga wanajulikana kwa uwezo wao mkubwa wa kufanya biashara na pia kilimo. Moshi ni maeneo ya mwanzo ambayo Wamisionari wa Ukristo walijenga makanisa na shule. Sababu hii imefanya Wachagga kuwa kabila lenye watu wengi zaidi walio na elimu ya kisasa na mkoa wa Kilimanjaro unaongoza kwa idadi ya shule za sekondari nchini Tanzania. Kulingana na takwimu za elimu mkoa wa Kilimanjaro una shule za sekondari zaidi ya 320. Pia mkoa una shule za msingi zipatazo 950. Idadi hii ya shule ni kubwa zaidi ya idadi ya shule katika mikoa mingine Tanzania. Shule nyingi za sekondari ziko katika mkoa huu kwa sababu zifuatazo: 1) Hali ya hewa na vivutio vya kitalii katika mkoa huu viliwavutia zaidi walowezi na wakoloni na kuweka makazi yao hapo. Hivyo wamisionari walijenga shule za kwanza wakifuatiliwa na serikali za wakoloni 2) Serikali ya Tanzania ilirithi shule zilizojengwa na wakoloni 3) Wachagga waliobahatika kupata fedha binafsi baadaye waliwekeza kwenye ujenzi wa shule binafsi kama kitega-uchumi, wakati wakazi wa mikoa mingine kadhaa walisubiri serikali iwajengee shule. 4) Ukichanganya sababu 1, 2 & 3 utagundua shule katika mkoa Kilimanjaro zimezidi sana idadi ya shule katika mikoa mingine yote. Ni vema pia kusema kUwa shule hizo huvutia wanafunzi kutoka Tanzania nzima, haziwasomeshi Wachagga tu. Kilimo na chakula Wachagga hulima mazao ya chakula kama vile mahindi, maharagwe, viazi, ndizi, ulezi na mboga mbalimbali. Pia mazao ya biashara kama vile kahawa, nyanya na vitunguu. Ndizi za Wachagga Ingawa Wachagga wa leo wanakula vyakula mbalimbali kama vile ugali, wali na viazi, chakula kikuu cha Wachagga ni ndizi. Kuna ndizi za aina mbalimbali na kwa matumizi tofauti. Mfano ndizi sukari ni fupi na huachwa hadi ziive na huliwa mbivu kama tunda. Ndizi mshale hukatwa zikiwa mbichi na kupikiwa vyakula mbalimbali pamoja na nyama ya ng'ombe, kondoo au mbuzi. Mara nyingine hupikwa na maharage, choroko, kunde au hata maziwa ya mtindi. Vyakula vya ndizi huja kwa ladha tofauti kama vile ndizi nyama, mtori, machalari, kiburu na kadhalika. Aina nyingine ni ndizi ng'ombe ambazo huachwa ziive halafu humenywa na kutumiwa kutengenezea pombe maarufu iitwayo mbege. Mbege hutengenezwa kwa kutumia ndizi mbivu, maji, na ulezi. Aina nyingine ni ndizi mzuzu. Hizi zikikomaa huachwa zianze kuiva kidogo halafu huchomwa na kuliwa kama kitafunwa pamoja na chai au pombe. Ukipita mitaa ya Dar es Salaam utaona ndizi mzuzu zikichomwa sambamba na muhogo au kuku vumbi au kiti moto. Wachagga na muhogo Inasemekana kuwa "Mchagga halisi hali muhogo - akila muhogo atakufa". Usemi huu umetokana na historia ya mababu kuwa Wachagga waliopanda mihogo Kilimanjaro enzi za kale walikufa baada ya kuila. Historia hiyo yaweza kuwa ya ukweli kwa sababu aina nyingi za mihogo zinajenga sumu ya sianidi ndani yake; watu waliozoea kutumia mihogo huwa na njia za kuondoa sumu kwa kuiloweka mihogo katika maji kwa muda. Lakini kama Wachagga wale wa zamani, hasa wa Machame, walifanya jaribio bila kujua mbinu ya kuondoa sumu, ajali iliweza kutokea. Cha kushangaza ni kwamba hukohuko Kilimanjaro, majirani na watani wa Wachagga, yaani Wapare, walikuwa wameshazoea mihogo na ilikuja kuwa moja ya chakula chao kikuu. Ulaji kiti-moto Pamoja na kilimo cha mazao, Wachagga hupendelea sana kufuga nguruwe. Tabia ya kula nyama ya nguruwe ijulikanayo leo kwa jina la "kiti moto" ni moja ya mambo yaliyoenezwa na Wachagga. Ulaji wa "kiti moto" haukuwa pendeza baadhi ya wenyeji wa Pwani kama Dar es Salaam ambapo Wachagga walihamia, kwani wakaaji wengi wa Pwani ni Waislamu kwa hiyo nguruwe kwao ni haramu. Wakazi wa Dar es Salaam watokao makabila mengine na wasiyo Waislamu kwao kula nguruwe ilikuwa "ruksa". Majina ya Kichagga Majina ya kiukoo ya Kichagga pia huashiria wanatoka sehemu gani ya Uchaga, japo si lazima kuwa hivyo: kwa mfano, familia maarufu za Kichagga nchini Tanzania ni kama ukoo wa akina Mushi, Kimaro, Swai, Massawe, Lema, Urassa, Nkya, Ndosi, Meena hutoka Machame. Akina Temu, Mlaki, Mlay, Lyimo, Moshiro, Mselle, Kamnde, Kileo, Kimambo, Tesha, Msaki, Assey, Kyara, Kessy, Ndanu, Macha, Mbishi, Kombe, Njau wanatoka Old Moshi na Vunjo. Kavishe, Mariki, Tarimo, Laswai, Mallya, Mrema, Mkenda, Massawe, Silayo, Lyaruu, Makyao, Mowo, Lamtey, Tairo, Mramba, Kauki wanatoka Rombo. Sawe, Usiri, Shayo, Kiwelu, Makundi, Urasa, Mtui, Moshi, Meela, Minja, Njau wanatoka Marangu na Kilema. Rite, Makule, Minja, Mashayo, Chao, Shao, Makawia, Ndesano, Kimario, Tilla, Mariale, Tarimo, Mafole, Kituo, Mrosso, Lyakundia, Kessy, Mmbando, Matemba, Ndenshau, Morio, Akaro, Matowo, Towo, Mkony, Temba Foya, Munishi, Kilawe na kadhalika hutoka Kibosho. Ukoo wa akina Teri wako Mamba, Chami, Chuwa, Kiria na wachache Sango, Old Moshi na wengine walihamia Maji ya Chai, Mkoa wa Arusha. Wachagga wengi hupenda kurudi nyumbani kipindi cha Krismasi, ikiwa ni kuwatembelea wazazi wao, rafiki, au ndugu. Ingawa wengi hudhani kwamba Wachagga wameathiriwa sana na dini ya Ukristo kwa kuwa wengi wao ni Wakristo na hiki huwa ni kipindi cha likizo kwao, inaaminika pia kuwa kurudi kwao Uchagani wakati wa Krismasi ni pamoja na kutembelea ndugu zao na kujumuika pamoja katika kuumaliza mwaka baada ya kazi nyingi za kutafuta pesa kwa mwaka mzima. Utawala wa jadi ya Wachagga Watawala wa Kichagga waliitwa "Mangi". Hawa walihodhi mashamba, ng'ombe na waliheshimiwa kama viongozi wa kikabila. Walikuwa na nguvu za kisiasa na utajiri. Baadhi ya Ma-mangi mashuhuri katika historia ni kama Mangi Rindi aliyeingia mikataba na wakoloni (Wajerumani), Mangi Sina wa Kibosho - anajulikana kwa uhodari wake wa vita katika kupigana na Wamachame na kupora ng'ombe na mazao yao na Mangi Marealle wa Marangu na Vunjo. Wakoloni walipokuja Kilimanjaro waliingia mikataba na viongozi hawa wa kikabila ili kuweza kuweka misingi yao ya kikoloni. Pia ndugu na watoto wa Ma-mangi walikuwa wa kwanza kupata elimu ya kikoloni, kwa hiyo waliweza kushirikishwa katika serikali za kwanza. Hawa pia wanaaminika walikuwa kama mabepari wa kwanza wa kijadi, maana walifanyiwa kazi na watu wengine wakati wao Ma-mangi wamekaa kuhesabu mali zao. Usemi maarufu wa "u-Mangi-meza" nadharia inawezekana kuwa umetokana na watawala hawa wa Kichagga. Ardhi Ingawa ardhi ni msingi wa maendeleo kwa watu wote, kwa Wachagga, ardhi ni mali sana kwa sababu kilimo chao ni cha mazao ya kudumu kama kahawa na ndizi hukaa shambani kwa muda wa miaka mingi. Mojawapo ya urithi wapewayo watoto ni "kihamba". Hii ni sehemu ya ardhi ambayo mtoto anategemewa atajenga na kuanzisha familia yake. Bahati mbaya watoto wa kike walikuwa hawapewi kipaumbele katika ugawanaji wa vihamba. Uhaba wa ardhi huko Uchaga ulipelekea Wachagga wengi kuhamia mikoa mingine. Hivi leo utakuta Wachagga wakiishi Dodoma, Morogoro, Iringa, Mbeya n.k. wakiwa wamepanda migomba yao na kuendesha biashara za maduka ya vyakula. Ukienda kwenye mikoa hiyo utakuta wamejenga jamii zao na vyama vyao vya kusaidiana wakati wa sherehe au matatizo. Aidha hata pombe ya mbege utaweza kuikuta kwenye makusanyiko ya Wachagga katika mikoa mbalimbali. Maoni juu ya Wachagga Ingawa wanaume wa Kichagga hupendelea kufanya kazi mbali na kwao, wake zao hukaa nyumbani (Moshi) na hufuga ng'ombe na kazi za shambani. ila kwa sasa kutokana na ugonjwa wa ukimwi tabia hii imepungua miongoni mwao. Wanawake wa Kichagga (hasa kutoka Rombo) hujulikana kama wafanyakazi hodari. Huchangia sana katika mapato ya nyumbani na chakula. Ingawa kipato cha Wachagga ni kikubwa kulingana na cha makabila mengine, takwimu zinaonyesha watoto wa mkoa wa Kilimanjaro kuongoza kwa utapiamlo. Sababu kubwa ya watoto kuwa na utapiamlo ni wazazi kujali zaidi kazi kuliko muda wa kuwahudumia watoto. Wengi wa watoto hao ni wale ambao wazazi wao ni watu wa pombe na kipato chao kinaishia kilabuni. Utaona kwamba Uchagga una vilabu vingi vya pombe na vinaongezeka kwa sababu imekuwa biashara kubwa. Karibu kila kaya kumi na tano kuna kilabu cha pombe na kiwango cha chini kabisa cha pombe inayouzwa kwa siku katika vilabu hivyo si chini ya madebe sita au lita mia moja. Pombe ni sababu moja ya watoto kuwa na utapiamlo. Hii inawezekana kuwa matunda ya wazazi kutowalisha watoto wao chakula cha kutosha au chakula bora. Kuna sehemu nyingine za Uchagga kama Old Moshi na Kibosho ambapo watoto wadogo hupewa pombe ya mbege asubuhi, mchana na jioni. Sababu nyingine ni kazi; mama wa Kichagga anaweza kushinda shambani kutwa na hana desturi ya kubeba watoto mgongoni kwenda nao shambani, hivyo wanakuwa nyumbani ama wenyewe au na mayaya. Mfano ulio dhahiri ni nyakati za asubuhi na mapema kwenye vyombo vya usafiri karibu robo tatu ya abiria ni wanawake wakienda katika shuguli za biashara na kilimo na vivyo hivyo nyakati za jioni wakirudi majumbani. Hao ni nje ya wale wanaotumia usafiri wa miguu ambao ni wengi zaidi. Pia baadhi ya kina mama wa Kichaga wanawajali waume zao zaidi kwani nyama nzuri ni ya baba. Kuepuka gharama baba ataandaliwa chakula kizuri, tofauti na chakula walichoandaliwa watoto, japo ni chakula kilekile. Pia Wachagga wamekua na desturi ya kuwaenzi wazee wao waliotangulia mbele za haki kwa kuwatambikia kwa pombe na nyama za mbuzi pale tu wanaporudi nyumbani ifikapo mwezi Desemba. Hili limekuwa suala la kawaida sana na halipingiki. Wengi wao huwa wanarudi na magari, ndiyo sababu utaona ya kwambwa kila ifikapo mwezi Desemba kila mwaka foleni za magari zimekuwa zikiongezeka kutokana na Wachagga kurudi nyumbani msimu wa sikukuu. Wengi wao wamekuwa wakitoka sehemu mbalimbali za nchi na hata nje ya nchi.

Sunday, 2 October 2016

SISI WANAUME BHANA... Mwanaume mmoja aliwatongoza wanawake watatu tofauti na nia yake ni kufanya upembuzi yakinifu ili mmoja wao awe mkewe. Hivyo jamaa aliamua kuwapa jaribio kwa kuwapa Tsh. 500,000/= kila mmoja huku akitaka kujua ni namna gani watazitumia. Mwanamke wa kwanza alitumia pesa yote kununua vipodozi. Alitembelea duka la vipodozi na urembo akajikwatua sawa sawa na kubust makalio! Alivyorudi kwa mchumba wake akamwambia, "Nimeamua kutumia pesa yote kwa ajili ya kujipamba ili nizidi kukupendeza machoni pako na kukuvutia maana nakupenda sana." Hakika yule mwanaume akapendezwa sana na mpenzi wake. Mwanamke wa pili alinunua zawadi kwa ajili ya bwana wake. Alinunua simu janja mpya kwa ajili ya bwana wake, saa ya kisasa, nguo na viatu vizuri. Alivyofika kwa bwana wake alimwambia, "Pesa yote nimeitumia kununua hizi zawadi zako maana nina kupenda sana." Jamaa akafarijika sana Mwanamke wa tatu aliwekeza zile pesa kwenye soko la hisa na baada ya muda fulani alipata faida ya shilingi 2,000,000/=. Mwanamke yule aliamua kumrudishia bwana wake ile pesa aliyokuwa amepewa yaani laki 5 na pesa iliyokuwa imebakia alifungua akaunti ya pamoja na bwana wake. Kisha yule mwanamke akamwambia yule jamaa, "Nahitaji kuwekeza na kuhifadhi kesho yetu kwa sababu nakupenda sana." Hakika yule mwanamke alimfurahisha sana jamaa. Jamaa akatafakari sana yale ambayo yalikuwa yamefanywa na wale wanawake baada ya kupewa laki 5. Lakini mwisho wa siku jamaa aliamua kumwoa mwanamke mwenye makalio makubwa! *Wanaume hatupendag ujinga sisi* 😂😂😂😂

Saturday, 1 October 2016

*GARI LA TAKA: PUNGA MKONO AGANA NAO* Siku moja nilichukua Tax na nilikuwa naelekea airport driver akiendesha kwa ustaarabu sana mara Ghafla pasipo tegemea Gari ya taka ikajitokeza mbele yetu toka ilipopaki DRIVER kwa umakini na NEEMA ya Mungu akalikwepa,na ilibaki kidogo agonge gari zingine mbele yetu. *PASIPO KUTEGEMEA DRIVER WA GARI LA TAKA AKAANZA KUFOKA NA KUPIGA KELELE HOPE UNAWAJUA WALE WATU!!* lakini driver alitabasamu na kuwapungia mkono nilishangaa sana na Kuumuliza inakuwaje ufanye hivyo wakat walitaka kutuua na hata kuharibu mali yako❓ *AKAJIBU KWA UPOLE AKINITAZAMA KWA TABASAM*😊 Akasema katika maisha yetu ,kuna watu wako kama gari la taka,wamejaa Stress,msongo,Hasira, maumivu,wamechoka kifikra,kiuchumi na kimaisha ,Masikitiko mengi, *SASA TAKATAKA ZAO ZINAZOPOWAZIDI HUTAFUTA MAHALI PA KUTUPA HAIJALISHI MAZINGIRA NA WATAKUTUPIA WEWE* Hivyo jfunze kutogombana nao Wapungie mkono, wape tabasamu songa mbele, haikupunguzii kitu kama haijakuumiza, usiruhusu wakupate na takakaka zao, HATA WEWE UMEKUTANA NAO WENGI,UNAPOTEZA MUDA WAKO,kuna wengine wanakulaani sana,kuna watu wanakusema mabaya na kukulaani wakati hufanyi ubaya ? Leo wapungie mkono na kumbuka neno hili Mith 26.2 *" 2 Kama shomoro katika kutanga-tanga kwake,Na kama mbayuwayu katika kuruka kwake;Kadhalika laana isiyo na sababu haimpigi mtu.* PUNGA MKONO/WAVE YOUR HAND YES JUST SMILE AND WAVE YOUR HAND TO THEM,DON'T ALLOW GARBAGE NEAR YOU WAVE NOW WAVE TODAY *MAISHA HAYA ULIUMBWA KUFURAHIA,USIYAFUPISHE KWA KUAMKA ASBH.NA KINYONGO,NA HASIRA,NA GHADHABU SABABU YA MTU,* SIKIA 1.WAPENDE NA WAFURAHIE WOTE WANAOKUTENDEA MEMA 2.WAOMBEE WOTE WANAOKUTENDEA MABAYA,wanaotaka kujaza taka na kuzimwa kwako KAMATA HII *LIFE IS 10% WHAT U MAKE IT* and and and *90% HOW U TAKE IT* *JIFUNZE KUJIFUNZA KUYACHUKULIA MAISHA KULIKO VILE UNAYATENGENEZA*by *HAVE GARBAGE FREE LIFE* *WITH LOT OF LOVE,WISH AND PRAYER PROSPERITY*

Tuesday, 27 September 2016

Ombi Ombi Ombi

*Ombi Ombi Ombi....* Maandiko yanasema Tafuteni nanyi mtapata, Ombeni nanyi mtapewa na Bisheni nanyi mtafunguliwa: Ndugu zangu kama kuna mdada ambae hajaolewa na anahitaji Mume tafadhali usikae kulia tuuu ukisubiri ule usemi wa ​mume bora anatoka kwa Bwana​ Huyu bwana ana njia nyingi za kumleta Mume sasa hebu njoo inbox

SHARE KWA MARAFIKI ZAKO HAPA

Popular Posts