Friday, 27 January 2017
MADHARA ya mionzi ya simu
Simu yako ni HATARI SANA kwenye Afya yako.
Fuhamu MADHARA yatokanayo na simu yako na JINSI YA KUYAPUNGUZA.
Simu tunazozitumia hutoa mionzi (radiations) hatari sana ijulikanayo kama "Electromagnetic waves" wakati wa kupiga/kupokea simu, kuperuzi Internet, nk..
Madhara ya Mionzi hii;
1. Husababisha Saratani ya Ubongo (Brain Cancer) na ngozi (Skin Cancer).
2. Husababisha hitilafu kwenye Ubongo na hii hupelekea kupoteza kumbukumbu, uwezo mdogo wa kupambanua mambo na umakini (Concentration).
3. Husababisha upungufu wa mbegu za kiume na hata utasa (Impotence) kwa wanaume.
4. Huongeza shinikizo la damu.
Jinsi ya kupunguza Athari zitokanazo na Mionzi hii hatari;
1. Weka vifaa maalum vya kupunguza mionzi (Radiation absorbers) kwenye simu yako. Vinapatikana madukani.
2. Usipende kuweka simu mfukoni endapo huitumii. Wakati wa kulala weka mbali angalao SM 30 kutoka ulipo.
3. Simu iwapo mfukoni, upande wa Vitufe na kioo cha simu ndio kielekee mwili wako!
4. Tumia "headsets" au "Kipaza sauti (Loud Speaker). Hii hukusaidia kuwa mbali na mionzi wakati wa kupiga/kupokea simu.
5. Usiitumie simu yako iwapo ina "bar" moja au mbili za "network" (Low Network Signal). Wakati huu simu inafanya kazi kupita kiwango cha kawaida hivyo huongeza wingi wa mionzi.
6. Wakati wa kupiga simu, subiri ipokelewe ndio uisogeze karibu ya mwili (mf. Masikioni).
7. Iwezekanapo, penda kuwasiliana kwa ujumbe wa maneno (text msg) kulipo kupiga simu.
Simu ni muhimu sana katika Maisha yetu ya sasa. Hutuunganisha na ulimwengu uliogubikwa na Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia.
Sanjari na hili, tunapaswa kuwa makini katika juhudi za kujaribu kuepuka Madhara yatokanayo na simu kama ilivyoainishwa hapo juu.
#plusJrPositeveMimd
NOTE: Share kwa wengine wajifunze.
Labels:
MAKALA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
SHARE KWA MARAFIKI ZAKO HAPA
Popular Posts
-
INTRODUCTION This work has contain four parts which are introduction that consist of meaning of the key terms, historical background of Leop...
-
Question: Discuss the role of Delegated Legislation in ensuring smooth administrative functions in Tanzania. 1.0 Introduction This work is...
-
INTRODUCTION. This document contains the definition of key terms which are natural justice, principle of natural justice andadministrative t...
-
COMMUNICATION AND INFORMATION SYSTEMS COMMUNICATION It is obvious fact that communication is such vital part of each of us that it contribut...
Unatusaidiaje sasa amabao tayari tumeshaathirika na hii mionzi ya simu
ReplyDelete