Showing posts with label HABARI. Show all posts
Showing posts with label HABARI. Show all posts

Sunday, 2 October 2016

Waziri Mkuu Ashangazwa Na Kodi Kubwa Soko La Dodoma.....Aagiza Baraza La Madiwani Lipitie Upya Na Kumpa Majibu MPEKUZI / 1 hour ago WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameliagiza Baraza la Madiwani la Manispaa ya Dodoma lifanye marekebisho ya kodi inayotozwa kwenye soko la Majengo ambayo imepandishwa kutoka sh. 20,000 hadi sh. 150,000 kwa mwezi. Amesema anatambua maamuzi ya Baraza ni ya kikao halali lakini hakubaliani na ongezeko hilo ambalo ni sawa na asilimia 650 kwani linawaumiza wananchi. Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana (Jumamosi, Oktoba Mosi, 2016) wakati alipotembelea soko hilo akiwa kwenye ziara ya kukagua maeneo ya kutolea huduma za jamii mjini Dodoma. Amesema soko hilo linatakiwa lifanyiwe mapitio ili liwekwe kwenye hali nzuri na Manispaa ihakikishe maboresho hayo yanafanyika bila ya kuwaumiza wafanyabiashara. “Kwa kuwa uamuzi wa kupandisha kodi ulifanyika kisheria na kupitishwa na baraza la Madiwani, sitaki kuvunja sheria. Nawaagiza mkazungumze tena katika baraza na muangalie namna ya kupunguza gharama hizo,” amesema. “Hali hii haiwezekani kuachwa iendelee, huku ni kuwaumiza wananchi. Mkurugenzi wa Manispaa nenda kaitishe tena kikao, mfanye mazungumzo upya kwenye baraza lenu na mje mnieleze mmekubaliana nini” amesisitiza. Pia ameitaka Manispaa hiyo ihakikishe makusanyo yote ya fedha katika soko hilo yanakusanywa kwa njia ya kielektroniki ili fedha hizo ziweze kuleta tija na kuwataka Mkuu wa mkoa na wilaya kuwachukulia hatua wotewatakaobainika kuiba fedha hizo. Amesema Manispaa hiyo inatakiwa kupanua masoko kwa kujenga masoko mapya makubwa katika maeneo ya Nkuhungu, Kisasa, Mlimwa na Barabara ya Iringa ili huduma hizo zisambazwe. Mapema akisoma risala yake, Mwenyekiti wa soko hilo, Bw. Godson Rugazama alimueleza Waziri Mkuu changamoto zinazolikabili soko hilo kuwa ni pamoja na ongezeko la kodi isiyozingatia uhalisia wa maisha na shughuli za wajasiriamali sokoni hapo. “Kodi imeongezeka kutoka sh. 20,000 hadi 150,000 kwa mwezi,” alisema. Mwenyekiti huyo alitaja changamoto nyingine ni uchakavu wa mifereji ya maji machafu, kuvuja kwa paa la soko, bidhaa kuuzwa katika maeneo yasiyokuwa rasmi na kusababisha wateja kutoingia sokoni. Wakati huohuo, Waziri Mkuu ametembelea hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma na kukagua maeneo mbalimbali zikiwemo wodi za wagonjwa, jengo la wazazi na jengo jipya la wagonjwa wa Bima ya Afya (NHIF). Akiwa hospitalini hapo, pia alizungumza na watumishi wa sekta ya afya na kuwataka wawahimize wananchi wajiunge na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ambao unawawezesha mtu kulipia bima ya matibabu kwa ajili ya mhusika, mwenza wake na watoto/watemezi wanne na serikali inajazia kiasi kile kile alichochangia. Akizungumzia miundombinu ya afya mkoani humo, Waziri Mkuu alisema mkoa wa Dodoma hauna shida ya matibabu au utoaji wa huduma ya afya kutokana na miundombinu iliyopo hivi sasa. Aliwataka wafanye kazi kwa uadilifu na uaminifu na kuongeza tija katika utendaji kazi wao huku wakitanguliza utunzaji wa mali ya umma. “Ninawasihi mjenge tabia ya huruma kwa wagonjwa huku mkitambua unyeti wa kazi mliyonayo. Ninaamini mtatunza vifaa mlivyonavyo na siyo kuvichukua na kuvipeleka kwenye zahanati zenu au maduka yenu binafsi ya dawa,” alionya. IMETOLEWA NA: OFISI YA WAZIRI MKUU
Bodi Ya Mikopo Ya Elimu Ya Juu Yatangaza Majina Ya Wanafunzi Waliokosea Kujaza Form Za Mikopo 2016/2017 MPEKUZI / 20 hours ago During the exercise of processing 2016/2017 loan application forms, the Board has come across loan applications which are missing some vital information such as applicant’s and guarantor’s signatures. For that reason, the Board would like to inform loan applicants with such incompleteness to visit HESLB offices in Dar es Salaam. Loan applicants and/or their guarantors who have not signed their documents are required to physically visit HESLB offices on Plot No. 8, Block No. 46 Sam Nujoma Road, Mwenge, Dar es Salaam to append signatures to their loan applications from Monday 3rd September 2016. Loan applicants who did not attach applicant’s photo, guarantor’s photo (to their application forms) or who attached uncertified photocopies of birth certificates, academic certificates, guarantor’s particulars such as photocopy of Passport or voter’s registration cards; should send the missing particulars with covering letters indicating their full names and form four index numbers with year of completion e.g. S0143.0012.2013 via EMS through the following address: The Executive Director, Higher Education Students’ Loans Board, P. O. Box 76068, DAR ES SALAAM. The deadline for correction of the shortcomings is Friday 7th October 2016. All attachments must be certified by a Commissioner of Oaths. NB: The Board is: • cautioning loan applicants to be careful with some unscrupulous individuals who might take advantage of this opportunity to make financial demands. •Reminding loan applicants that correction of missing items is not a guarantee to be awarded loans. • Incomplete application forms will not be considered for further processing until the missing information is provided within specified time. *The list of loan applicants with missing signatures and other attachments can be viewed through: http://olas.heslb.go.tz

Saturday, 1 October 2016

Tangazo kwa wanafunzi wote college of humanity and social science and college of business and law. Kutokana na mgawanyo wa college ambao upo utaratibu utakuwa kama ufuatavyo kwa upande wa makazi kwa mwaka wa masomo 20 16/2017, wanafunzi wote wa college of humanity and social science wataishi kuanzia block namba 1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8, 9, 10, 11 na 12. College of business and law kuanzia block namba 13, 14, 15, 16, 17, 18 na 19. Hivyo basi kutokana na mgawanyo huo utaanza kipindi hiki cha mtihani ya supplementary na special exams. Wanafunzi wote ambao wataenda kufanya supplementary na special exams wanatakiwa waende ktk blocks zao kulingana na college yako na course unayosoma. Note: mgawanyo huo hauhusiani na serikali ya wanafunzi itaendelea kubaki vile vile hadi mwezi wa tano 2017 wakati wa uchaguzi, kwa upande wa block leaders wote wataendelea kubaki pale pale kwenye block zao haitojalisha course wala college unayosoma. Imetolewa na waziri wa makazi, maji, ulinzi na usalama. Juma Juma M. 0656 0656 46.
*BREAKING NEWS* *BODI YA MIKOPO IMETANGAZA MAJINA YA WANAFUNZI FORM 6 NA DIPLOMA WALIOKOSEA KUJAZA FORM ZA MIKOPO 2016/2017* *DEADLINE YA KUFANYA MASAHIHISHO NI TAR 7/10/2016* *TAFADHALI TUMA KWENYE MAKUNDI YAKO 10 TU WAPATE TAARIFA HII MUHIMU* *MASWAYETU BLOG,TUNAKUPENDA SANA😘* kuona majina hayo bonyeza hapo>>>>> www.maswayetublog.com/2016/10/mpyahaya-hapa-majina-ya-wanafunzi.html

Tuesday, 27 September 2016

Ombi Ombi Ombi

*Ombi Ombi Ombi....* Maandiko yanasema Tafuteni nanyi mtapata, Ombeni nanyi mtapewa na Bisheni nanyi mtafunguliwa: Ndugu zangu kama kuna mdada ambae hajaolewa na anahitaji Mume tafadhali usikae kulia tuuu ukisubiri ule usemi wa ​mume bora anatoka kwa Bwana​ Huyu bwana ana njia nyingi za kumleta Mume sasa hebu njoo inbox

SHARE KWA MARAFIKI ZAKO HAPA

Popular Posts