Showing posts with label BIBLE. Show all posts
Showing posts with label BIBLE. Show all posts

Wednesday, 14 December 2016

Sala mbali mbali

SALA YA ASUBUHI. Kwajina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina. Ee Baba yetu Mungu mkuu, Umenilinda usiku huu. Nakushukuru kwa moyo, Ee Baba, Mwana na Roho. Nilinde tena siku hii, Niache dhambi, nikutii. Naomba sana Baba wee, Baraka zako nipokee. Bikira safi, Ee Maria Nisipotee nisimamie. Mlinzi mkuu malaika wee, Kwa Mungu wetu niombee Nitake nitende mema tu, Na mwisho nije kwako juu. Amina. NIA NJEMA. Kumheshimu Mungu wangu Namtolea roho yangu, Nifanye kazi nipumzike Amri zake tu nishike Wazo, neno, tendo lote Namtolea Mungu pote Roho, mwili chote changu, Pendo na uzima wangu Mungu wangu nitampenda, Wala dhambi sitatenda. Jina lako nasifia, Utakalo hutimia. Kwa utii navumilia Teso na matata pia. Nipe, Bwana, neema zako Niongeze sifa yako. Amina. SALA YA MATOLEO. Ee Yesu, kwa mikono ya Bikira Maria, na kwa maungano na sadaka yako kuu, ninakutolea sala, matendo, masumbuko na furaha zangu zote za leo. Ee Yesu, ufalme wako utufikie. BABA YETU. Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi, lakini utuopoe maovuni. Amina. SALAMU MARIA. Salamu, Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria Mtakatifu mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina. KANUNI YA IMANI. Nasadiki kwa Mungu Baba mwenyezi. Muumba wa Mbingu na dunia. Na kwa Yesu Kristo Mwanae wa pekee, Bwana wetu. Aliyetungwa kwa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria. Akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato. Akasulibiwa, akafa, akazikwa; akashukia kuzimu. Siku ya tatu akafufuka katika wafu. Akapaa mbinguni, amekaa kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi. Toka huko atakuja tena kuwahukumu wazima na wafu. Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Kanisa takatifu katoliki, ushirika wa watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miili na uzima wa milele ijayo. Amina. AMRI ZA MUNGU. 1. Ndimi Bwana Mungu wako, usiabudu Miungu wengine. 2. Usilitaje bure jina la Mungu wako. 3. Shika kitakatifu siku ya Mungu. 4. Waheshimu Baba na Mama upate miaka mingi na heri duniani. 5. Usiue. 6. Usizini. 7. Usiibe. 8. Usiseme uongo. 9. Usitamani mwanamke asiye mke wako. 10. Usitamani mali ya mtu mwingine. AMRI ZA KANISA. 1. Hudhuria misa takatifu, dominika na sikukuu zilizoamriwa. 2. Funga siku ya jumatano ya majivu; usile nyama siku ya ijumaa kuu. 3. Ungama dhambi zako walau mara moja kila mwaka. 4. Pokea Ekaristi takatifu hasa wakati wa Paska. 5. Saidia Kanisa katoliki kwa zaka. 6. Shika sheria katoliki za ndoa. SALA YA IMANI. Mungu wangu, nasadiki maneno yote. Linayosadiki na linayofundisha Kanisa Katoliki la Roma. Kwani ndiwe uliyetufumbulia hayo. Wala hudanganyiki, wala hudanganyi. Amina. SALA YA MATUMAINI. Mungu wangu, natumaini kwako, nitapewa kwa njia ya Yesu Kristo. Neema zako hapa duniani, na utukufu mbinguni. Kwani ndiwe uliye agana hayo nasi, nawe mwamini. Amina. SALA YA MAPENDO. Mungu wangu, nakupenda zaidi ya chochote. Kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza. Nampenda na jirani yangu, kama nafsi yangu, kwa ajili yako. Amina. SALA YA KUTUBU. Mungu wangu, nimetubu sana dhambi zangu. Kwani ndiwe mwema, ndiwe nwenye kupendeza. Wachukizwa na dhambi, basi sitaki kukosa tena. Nitafanya kitubio, naomba neema yako, nipate kurudi. Amina. SALA KWA MALAIKA MLINZI. Malaika mlinzi wangu, unilinde katika hatari zote, za roho na za mwili. Amina. MALAIKA WA BWANA Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria. Naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Salamu, Maria,..... Ndimi mtumishi wa Bwana. Nitendewe ulivyonena. Salamu, Maria.... Neno la Mungu akatwaa mwili. Akakaa kwetu. Salamu, Maria.... Utuombee, Mzazi mtakatifu wa Mungu. Tujaliwe ahadi za Kristu. Tuombe Tunakuomba, Ee Bwana, utie neema yako mioyon mwetu, ili sisi tuliojua kwa maelezo ya Malaika kwamba Mwanao amejifanya mtu kwa mateso na msalaba wake tufikishwe kwenye utukufu na ufufuko. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu. AMINA.. ATUKUZWE (mara tatu) Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. Kama mwanzo na sasa na siku zote na milele. Amina. Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.

Sunday, 9 October 2016

Nmefufuliwa na bwana

πŸ™‡�πŸ™‡Neno la� Bwana lasema.... Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu. Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu; kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu. Katika hayo ninyi nanyi mlitembea zamani, mlipoishi katika hayo. Lakini sasa yawekeni mbali nanyi haya yote, hasira, na ghadhabu, na uovu, na matukano, na matusi vinywani mwenu. Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale, pamoja na matendo yake; mkivaa utu mpya, unaofanywa upya upate ufahamu sawasawa na mfano wake yeye aliyeuumba. Hapo hapana Myunani wala Myahudi, kutahiriwa wala kutokutahiriwa, mgeni wala mshenzi, mtumwa wala mwungwana, bali Kristo ni yote, na katika yote. Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi. Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu. Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani. Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.πŸ™‡�πŸ™‡�πŸŒπŸ“ƒ. .Wakolosai 3:1.............

Monday, 3 October 2016

Yohana 3:16

Tumsifuni Yesu kristo... Mungu ni Mwema ..Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜† Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. πŸ™‡ πŸ™‡ πŸ™‡ Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.πŸ™ πŸ™ .. Yohan3:16....

Meno la mungu

Nawasalim katika jina la Bwana .karibu tena katika Neno la Mungu.. ..Mitume wakamwambia Bwana, Tuongezee imani. Bwana akasema, Kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu huu, Ng’oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii. Lakini, ni nani kwenu mwenye mtumwa alimaye au achungaye ng’ombe, atakayemwambia mara arudipo kutoka shambani, Njoo upesi, keti, ule chakula? Je! Hatamwambia, Nifanyie tayari chakula, nile; jifunge unitumikie, hata niishe kula na kunywa, ndipo nawe utakapokula na kunywa? Je! Atampa asante yule mtumwa, kwa sababu ameyafanya aliyoagizwa? Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya. Amina kama umelielewa neno hakika utakua umejifunza kitu kipya...Tutafakari pamoja..luka 17:5---10.....

SHARE KWA MARAFIKI ZAKO HAPA

Popular Posts