Wednesday 14 December 2016

Historia ya uhuru wa tz

Ukweli umefichuka, historia ya uhuru wa Tanganyika By. @SANGAPIPI JF Senior Member #1 3 minutes ago Joined: Jun 25, 2013 Kwamujibu wa John Silivalon katika kitabu chake anabainisha nguvu ya kanisa katika siasa ya Tanzania, Lakini John sio yeye tu, @Yericko Nyerere pia katika kitabu chake kiitwacho Ujasisi wa Kidola na Kiuchumi Sura ya Pili, uk 295, ameeleza kwakirefu... Nanukuu "Maamuzi yoyote ya mwelekeo wa dunia hutokea baada ya kukubaliwa ama kuratibiwa na Kanisa kupitia shirika la Jeisuti ambalo utendaji wake ni wa siri zaidi. Karne ya 17 kanisa lilikuja na mpango madhubuti wa kuisaka haki ya kibinadamu katika ulimwengu wa kikoloni, ijapokuwa mpango huo ulikuwa ukibadilika malengo kila nyakati kulingana na mahitaji ya karne. Baada ya vita vya kwanza vya dunia, Shirika la Wajeisuiti lilikuwa na nguvu na lilikuwa tayari sehemu ya tawala nyingi duniani hivyo kufanya kisiwepo kitakachofanyika bila majasusi hawa kujua ama kuhusika, hasa juu ya mstakabali wa dunia ijayo, walikuwa na bado wanauoni mkubwa wa mambo yajayo. Wazo la kuwa na Shirikisho la Mataifa lilitolewa mara ya kwanza na mwanafalsafa Mjerumani Immanuel Kant mnamo mwaka 1795. Wazo la Kant lilirudiwa na wanafalsafa mbalimbali. Wakati wa vita kuu ya kwanza rais wa Marekani Woodrow Wilson alipendekeza hatua za kuanzisha shirikisho hili kwa kusudi la kuzuia vita za wakati ujao baada ya mwisho wa vita ile. Kant alikuwa wakala wa ujasusi wa Wajeisuiti akiripoti kwa Karl Theodor von Dalberg, alizaliwa mjini Königsberg (sasa: Kaliningrad) 22 April 1724 kama mtoto wa fundi. Mamake alimsomesha kweye shule ya sekondari akaendelea kusoma theolojia, falsafa, sayansi, fizikia na hisabati. Tasnifu (thesis) yake ya kwanza haikupokelewa na profesa wake mwaka 1746 hivyo alifanya kazi ya ualimu kwenye nyumba ya matajiri na makabaila mbalimbali kwenye mazingira ya Königsberg. Mwaka 1754 alirudi kwenye chuo kikuu akamaliza masomo yake. Tangu 1755 alikuwa mwalimu na tangu 1870 profesa kamili kwenye chuo kikuu cha Königsberg.Hakuoa aliishi na mtumishi wa nyumbani tu hadi kifo chake mwaka 1804 kwa umri wa miaka 80. Kaburi lake ni kando la kanisa kuu la Königsberg limetunza hata siki hizi baada ya kufukuzwa kwa Wajerumani na kuwa sehemu ya Urusi. Katiba ya shirikisho la mataifa ilikuwa sehemu ya mkataba wa Versailles mwaka 1919. Nchi washindi au mataifa ya ushirikiano zilijiunga na umoja huo mpya. Baada ya kukubaliwa na nchi za kutosha shirikisho lilianza rasmi tarehe 10 Januari 1920.Katiba ilikuwa na madhumuni kama yafuatavo: Fitina zote kati ya nchi zitasuluhishwa kwa njia ya amani kwa azimio ya kamati au mahakama ya kimataifa. Nchi wanachama zote zitaungana dhidi ya nchi yoyote itakayoanzisha vita mpya au kukataa azimio la mahakama ya kimataifa. Nchi zinapatana kupunguza jeshi zao na idadi ya silaha zilizopo Mkutano mkuu wa. Kamati kuu au halmashauri ya nchi wanachama nne (baadaye sita)na nafasi nne (baadaye 9) za nchi zinazobadilishana kwa zamu. Ofisi kuu inayoongozwa na Katibu Mkuu Mahakama ya kimataifa inaundwa ya kutoa azimio katika matatizo kati ya madola. Mkataba wa Versailles ulianzisha aina mpya ya maeneo yaliyowahi kuwa ama koloni au majimbo ya nchi zilizoshindwa katika vita. Koloni zote za Ujerumani pamoja na sehemu kubwa ya majimbo ya Milki ya Osmani ya awali ziliwekwa chini ya mamlaka ya Shirikisho la Mataifa na kukabidhiwa kwa nchi washindi wa vita. Zilipewa hali ya pekee kama maeneo ya kudhaminiwa. Tofauti na koloni za kawaida nchi wadhamini hazikupewa mamlaka yote jinsi iliyokuwa katika koloni zao za kawaida bali zilipokea maeneo ya kudhaminiwa chini ya masharti fulani pamoja na kulinda haki kadhaa za wenyeji na KUZIANDAA nchi hizi kwa uhuru. Hapo mwanzoni tofauti kati ya koloni na eneo la kudhaminiwa haikuwa kubwa lakini baadaye masharti ya udhamini yalikuwa muhimu. Kwa mfano hali ya Tanganyika kuwa eneo ka kudhaminiwa ilisababisha Uingereza kutokubali walowezi wengi kuja hapa. Vivyo hivyo hali ya Afrika ya Kusini Magharibi kuwa eneo la kudhaminiwa ilizuia sehemu hii kuwa jimbo la Afrika Kusini kuwa msingi kwa uhuru wake kama nchi ya Namibia. Jukumu la kuandaa nchi hizo kupata uhuru liliratibiwa na shirika hilo la kijasusi kwa ustadi mkubwa bila baadhi ya makoloni kujua, lakini lilikumbana na kikinza hasa kufuatia mnyumbuliko wa kiimani ndani ya ukristu kufuatia nguvu ya Cambrige (Anglikana), mgogoro huo ulikuzwa kwakuwa Anglikana nao tayari walikuwa wameaandaa taasisi yao waliyoiita Fabian Sociaty maalumu kwaajili ya kuwaandaa vijana wa kiafrika kukabidhiwa nchi zao, Barani Afrika Jeisuiti ilibadili mbinu kwakuwa dola la Kiingereza lilikuwa kikwazo kwa sehemu fulani, haikujikita kwenye dola isipokuwa ilisimama katika muundo wa shirika lifanya shughuli zake ndani ya Kanisa. Dhamiri ilikuwa lazima itimie, kama ilivyosemwna huko mwanzo kuwa hawa ndio wabobevu wa elimu ya juu kwa kila nyanja na ndio wanaotawala ulimwengu, hivyo vikwazo havikukwamisha wao kufikia malengo. Katika Tanganyika chini ya Udhamini wa Jumuiko la Kimataifa, kulikuwa na harakati za hapa na pale za kudai haki za kiraia kwa wenyeji. Ifahamike kuwa vyama vya harakati hizo Tanganyika vilikuwa vingi sana, na vipo vilivyokuwa vikipingana vyenyewe kwa vyenyewe. Mwaka 1927 hadi 1929 kanisa Katoliki nchini chini Joseph Gabriel Zelger, lilibainika kuingiza siasa katika utendaji kazi zake, kitendo hiki kiliwakwaza wakuu wa mamlaka ya kikoloni na kupelekea majasusi wakikoloni wapendekeze aachishwe uongozi wa kanisa nchini. Ni kweli tarehe 12 februari 1929 Zelger alistaafu wadhifawake kwa lazima. Ni mwaka huohuo wa 1927 ndio Chama cha African Assosiotion (AA) kilianzishwa na Gavana Sir David Cameron maaluma kwaajili ya kuratibu sherehe za watu weusi huko pembeni ya mji huko mtaa wa Stanley (leo Lumumba) na kuwapa ofisi mahali leo wanapojiita TANU ilizaliwa. Lakini historia ya Tanganyika haiwataji waasisi wa AA, Rais wa kwanza Mwalimu Cesil Matola (msomi wa mwanzo kabisa enzi za mjerumani kutoka kabila la Wayao), katibu mkuu wa kwanza Klest Sykes (Mzulu Baba yake alikuwa mateka wa kikoloni toka Afrika Kusini), Mwekahazina Ali Ramadhan (mzaramo na mvuvi maarufu wa pwani la Azania). Hao ndio mwaka 1927 waliounda Chama cha kwanza kabisa cha kutetea maslahi ya weusi Tanganyika na shughuli zake zilikuwa ni kuratibu sherehe za waafrika tu. (Chama cha walevi kwa lugha nyingine). Mwaka 1933 Mwalimu Cesil Matola alifariki na nafasi yake ikakaimiwa na katibu mkuu wa chama hicho bwana Klest, mpaka ilipofika mwaka 1948 yakatokea mapinduzi yaliyoongozwa na mtoto wa Klest aliyeitwa Abdulwahid Sykes huyu alikuwa ametoka kupigana vita vya pili vya dunia huko Burma, na aliporudi alikuwa na mawazo ya ujana toka vitani, akampindua baba yake kwa kumpiga ngumi puani, mapinduzi yaliyoitwa “ondoa wazee”. Kisha AA ikabadilishwa jina na kuitwa TAA, Rais wake wa Kwanza akawa Dr Vedasto Kyaruzi (Mhaya), huyu ndie dakitari wa binadamu wa kwanza kabisa wa kiafrika Tanganyika, Katibu mkuu akawa Abdulwahid Sykes na Mweka hazina akawa Dosa Azizi, utawala huo ulienda mpaka mwaka 1953 uchaguzi ulipofanyika na Nyerere akashinda pale kwenye ukumbi wa Anautoglo Mnazimoja leo, mwaka 1954 Nyerere akabadili jina la chama na kuwa TANU jina ambalo lilibuniwa na Abdulwahid Sykes, TANU ilikwenda mpaka mwaka 1977 na kisha kikazaliwa chama kiitwacho CCM baada ya Muungano wa ASP na TANU. Kisa hiki cha kufukuzwa kwa Kasisi huyu Bw. Zelger kinasema, Kanisa lilianzisha mafundisho yenye kuchochea fikra za kimaasi, nalilifanikiwa kuandaa wakufunzi maalumu kwenda katika majimbo yote ya kihuduma Tanganyika, hilo lilipelekea kuleta mtafaruku na dola ya mkoloni wa kiingereza ambapo ilimgharimu kiongozi huyu wa kiroho kuachia madaraka yake. Alipoingia askofu Edger Aristide Maranta mwaka 1930, ikiwa kama vile mwendelezo wa mtangulizi wake, Askofu Maranda alianzisha harakati za kuwashawishi viongozi wengine wa majimbo kuendeleza kutoa mafundisho yenye kumfanya mtanganyika ajitambue na adai uhuru wake, mfano, 23 mei 1938 wakati makanisa saba ya Kilutheri yakiwa kwenye hatua za mwanzo za mchakato wa kuungana, Askofu maranda aliomba kuhudhuria kikao cha tarehe 8 mwezi wa sita kilichofanyika Mjini Arusha, Askofu Maranda aliudokeza mpango ule wa siri wa katoliki katika kikao hicho, japokuwa kulikuwa na hofu ya kutoaminiana, lakini uthabiti wa malengo hayo ulijipembua baadae na kuwa wamafaa, ushahidi wa nyaraka za kumbukumbu za mkutano huo unaeleza. Juhudi za kanisa kupigania mkataba wa Versailles ziliendelea kushika kasi huku zikiendeshwa kwa siri sana kwamfumo wa neno la kiroho, na ilipofikia miaka ya 1950+ kanisa sasa lilikuwa tayari linanguvu ya ushawishi kufuatia mafanikio ya harakati za kanisa katika nyanja za ukombozi barani afrika. Wakati hayo yakiendelea tayari kanisa kupitia shirika lake la kijasusi lilikuwa limewekeza kwa nguvu kubwa kumtafuta mtu imara mwenye weledi na vipawa atakayejengwa ili aje kuongoza nchi. Mtihani mkubwa kwa kanisa ilikuwa ni namna gani linaweza kuingia rasmi kudai uhuru wa Tanganyika. Katika kipindi hiki tangu harakati za kanisa zianze, Askofu Maranta pamoja na mapadre wa baadhi ya mikoa, walikuwa tayari ameshafanya juhudi kadhaa za kukutana na Mashehe waliokuwa na ushawishi mkubwa, mfano 05/02/1948, Askofu Maranda alikutana Shehe Issa bin Amir kiongozi wa kiroho katika msikiti wa Ilala - mchikichini. Shehe Issa Bin Amir alizaliwa 1846 katika viunga vya Mzizima, mchikichini na kuhudumu katika wadhifa wa shekhe katika msikiti uliokuwa hapohapo viwanja vya nyumbani kwake na alifariki mwaka 1953 akiwa na umri 107, Shehe Issa Bin Amir kwa kabila alikuwa Mzaramo na akiishi hadi kifo chake Mchikichini pale nyuma ya kilipo kiwanda cha bia leo (TBL). Shehe Issa Bin Amir rafiki kipenzi wa Padre Maranta na mzee wa hekima za kilele cha zama hizo, mtu aliyekuwa kiungo muhimu kati ya uislamu na ukristu, Mtu ambae Mwalimu Cesil Matola rais wa kwanza wa AA na Klest Sykes katibu mkuu wakwanza wa AA, na wanachama wengine waliokuwa AA walimheshimu sana kwa hekima zake na mmoja wa wasisi wa Jumuiko la Uislamu Afrika Mashariki (EAMWS) Mazungumzo yao yalihusu harakati za ukombozi, Shehe Issa alimshauri Askofu kuwa ikiwa makanisa na misikiti yanapigwa marufuku na mkoloni kujihusisha na siasa za ukombozi basi watafute baadhi ya vyama vya harakati za ukombozi na waviunge mkono, wazo hilo lilimvutia Askofu lakini akajenga hofu kama je ndani ya vyama hivyo watapata vijana wasomi?. Siku chache baada ya makutano yake na Shehe Issa, Askofu Maranta aliletewa mapendekezo kutoka kwa Attilio Beltramino kasisi wa katoliki aliyehudumu kule Iringa, mapendekezo ya kasisi huyu yalikuwa ni, Umishonari makao makuu uruhusu udurufu wa biblia zisomeke kwa makabila ya wahusika wa eneo, ndani ya biblia hizo yaongezwe mafundisho ya haki ya kujitambua na kujitawala wenyewe. Pendekezo hili lilimvutia sana Maranta hivyo akalipa baraka zake, kwa hakika lilifanikiwa na ndio lilizaa hisia kali za mwamko wa kudai uhuru, mfano biblia ya lugha ya kihehe ilikuwa inaeleza wazi athari za kutawaliwa. Harakati za Ukombozi za Mwalimu Nyerere akiwa na nguvu mpya ya kifikra toka Chuo kikuu, zililivutia kanisa na uungaji mkono ukachagizwa, mfano mwaka 1953 wakati TAA kikiwa chama chenye nguvu kufuatia mabadiliko ya 1948 toka AA kwenda TAA. Askofu Maranta alimwalika ofisini kwake Mwalimu Nyerere, walizungumza mengi lakini kubwa nikuwa alimsifu kwa juhudi za kujipambanua bila kuwaogopa wakoloni, akamweleza jinsi kanisa linavyounga mkono juhudi za ukombozi wa Tanganyika, kisha akamshauri kuwa ajaribu kuvishawishi baadhi ya vyama vya harakati za kiraia viungane ili kuvipa nguvu ya kudai uhuru na kanisa litasaidia. Wazo la Askofu Maranta lilimkaa Mwalimu Nyerere na mwaka 1954, alianza juhudi za kuwaunganisha vijana wenzake wa kariakoo ambao walikuwa ndani ya TAA na wenye nguvu ya ushawishi lakini wakikabiliwa na matatizo makubwa mawili katika lengo lao ambayo ni Elimu na Woga. Ikumbukwe kuwa mwaka 1953 baada ya harakati za ukombozi kupamba moto na kamata kamata ya wanaukombozi, Askofu Edger Aristide Maranta alihamishiwa Zanzibar na nafasi yake ikachukuliwa na Vicar Apostolic, lakini bado aliendelea kuwa mshauri imara wa Mwalimu Nyerere. Jambo la kushangaza kama si kufurahisha, mwaka huohuo mwezi wa 8, Edger Aristide Maranta alirudishwa tena Dar es Saalam, na sasa mbinyo dhidi ya ukoloni ukashika mkondo wake. Mnamo tarehe 07/07/1954, Vijana (wazee wa kariakoo) wakiongozwa na Julius Kambarage Nyerere, walikubaliana wazo la kuhuisha chama kutoka TAA kwenda TANU, chini ya uratibu wa karibu wa Wajeisut (Askofu Maranta) na Waislamu (Shehe Issa bin Amir) ijapokuwa alikuwa amefariki mwaka mmoja nyuma, lakini hekima za Shehe huyu zilisaidia. Na zaidi ni kuwa safari ya kwanza ya Mwalimu Nyerere ya kwenda UNO 05/03/1955 Kanisa Katoliki lilitoa msaada kwa chama cha TANU wa tiketi ya ndege ya kwenda na kurudi, lilifanya hivyo kupitia shirika lake la Maryknoll Sisters la New York Marekani, Si hivyo tu bali katika moja ya utani wa Mwalimu wenye ukweli ndani yake aliwahi kusema kuwa makasisi Walsh na Art Wille wa Shirika la Maryknoll ni maboss wake, akikumbuka malipo ya shilingi 600 angali ameacha kazi ya ualimu akiwa kijijini Butiama.Kuna ushahidi wa kihistoria pia unaochagiza habari hizi kwamba majasusi wa Kanisa walimuandaa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuja kuwa kiongoza Tanganyika mpya. Barua ya lugha ya kilantini ya kitume TOT TANGAEQUE ya 8 Novemba 1984 ya Papa wa Roma kwenda kwa Kanisa la Katoliki Tanzania inautangazia ulimwengu kwamba Tanzania itakuwa chini ya himaya ya kanisa kwa mwavuli wa Bikira Maria Imakulata." NB Nashukuru sana kuona watu wanasoma na kuthamini kazi yangu nakuitumia kama rejea katika maandishi yao....

No comments:

Post a Comment

Show your comments here

SHARE KWA MARAFIKI ZAKO HAPA

Popular Posts