Sunday, 23 October 2016

Baada ya mwanamke kukataa kufungua mlango angalia kilichomkuta

Walevi hatupendagi ujinga kabisa Nyumba ya mlevi mmoja nje kuna shimo kubwa la maji bila mfuniko. Siku moja karudi usiku kalewa tooooop, mambo yakawa hivi: *MUME*: Fungua mlango! *MKE*: Leo sifungui! Nimechoshwa na ulevi wako. *MUME*: kama hufungui najitupa kwenye hili shimo nife kabisa. *MKE*. Kufa huna faida yoyote duniani! *MUME* kachukua jiwe kubwa kalitupa kwenye shimo chubwiiiiiii! MKE kajifunga kanga, kafungua mlango. Ghafla mume kaingia ndani na kumfungia mke nje. *MKE*: Nifungulie la sivyo nitapiga kelele majirani waje. *MUME*: Piga kelele na wakija uwambie unakotoka usiku huu na khanga moja.

No comments:

Post a Comment

Show your comments here

SHARE KWA MARAFIKI ZAKO HAPA

Popular Posts