Sunday, 9 October 2016

Mapya ni mapenzi

090 - Mapya Ni Mapenzi 1 Mapya ni mapenzi hayo,, asubuhi tuonayo, Saa za giza hulindwa, kwa uzima kuamka. 2 Kila siku mapya pia, rehema wema na afya, Wokovu na msamaha, mawazo mema furaha. 3 Tukijitahidi leo, na mwendo utupasao, Mungu atatueleza, yatakayompendeza. 4 Mambo yetu ya dunia, Bwana atayang’aria, Matata atageuza, yawe kwetu ya baraka. 5 Yaliyo madogo haya, Bwana tukimfanyia, Yatosha tutafaidi, huvuta kwake zaidi. 6 Ewe Bwana siku zote, tusaidie kwa yote, Mwendo wetu wote vivyo, uwe kama tuombavyo.

No comments:

Post a Comment

Show your comments here

SHARE KWA MARAFIKI ZAKO HAPA

Popular Posts